Asema kuwapa uongozi Chadema ni sawa na kumkabidhi Bucha Fisi
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetaka Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha
Katoro Mazemule na wenzake wanaodaiwa kuhusika na wizi wa sh. milioni
16.5 za Halmashauri ya kijiji hicho wafikishwe mahakamani haraka.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara leo, katika mji mdogo
wa Katoro, mkoani Geita, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
alisema, ni lazima wahusika wote wa wizi wa fedha hizo wafikishwe
mahakamani kwa kuwa ni jasho la wananchi.
Fedha hizo zinadaiwa kuliwa na Mwenyekiti huyo kwa
tiketi ya Chadema, katika kipindi cha mwaka 2010 na 2011 hali ambayo
imezusha tafrani miongoni mwa wananchi na uongozi wa Halmashauri ya
Kijiji hicho hadi sasa.
Nape alisema, ni lazima Mwenyekiti huyo na
waliohusika wote wafikishwe mahakamani kwa kuwa kamati iliyoundwa
kuchunguza upotevu wa fedha hizo ilishamaliza kazi yake na ripoti
kukabidhiwa kwa mamlaka zinazohusika.
"Kamati ya kuchunguza wizi wa fedha hizi ambazo ni
mali ya wananchi ilishafanya kazi yake na kukabidhi ripoti kwa mamlaka
zinazohusika, sasa kinachosubiriwa ni nini wahusika hawa kupelekwa
mahakamani?", Nape alihoji na kuongeza;
"Sasa CCM kwa kuwa ndicho chama tawala, tunaagiza
hatua za kuwapeleka mahakamani wahusika wote zichukuliwe haraka ili haki
itendeke".
Nape alisema, kutotokea kwa wizi wa
fedha hizo chini ya uongozi wa Halmashauri ya Kijiji hicho ambao upo
chini ya chama hicho, ni dalili kwamba kujidai kwao kuwa wasafi na
wapigania haki za wanyonge ni sawa na kilio cha mamba.
" Kila mara tumekuwa tukiwaambia acheni kuhadaiwa na
Chadema, hawa siyo chama cha siasa ni kundi la wajanja fulani, sasa
Wana Katoro mmejionea wenyewe, mmewajaribu mkawapa halmashauri yenu,
fedha wamezitafuna sasa mnahangaika", alisema na kuongeza;
"Kwa kuwa mmepata funzo hili, bila shaka hamtaruidia
tena, kwani mmeshafahamu kwamba kuikabidhi uongozi Chadema ni sawa na
kumkabidhi fisi bucha".
Mapema, Mwenyekiti wa
CCM mkoa wa Geita, Joseph Msukuma, alisema kwenye mkutano huo kwamba,
kama hatua za kuwafikisha mahakamani wahusika hazitachukuliwa haraka,
ataongoza wananchi wa Katoro kuandamana ili kuhakikisha hatua hizo
zinachukuliwa.
Kabla ya mkutano huo, NMape alifungua shina la
wajasiriamali la CCM, Bugayambele lenye wanachama 53 ambao hushughulika
na kazi za kutengeza fenicha mbalimbali katika karakana yao iliyopo
eneo hilo la Katoro.
Akifungua shina hilo, Nape aliahidi kuwapa sh.
milioni moja kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao, ikiwa ni pamoja na
kununua vitendea kazi kama randa za mbao, mashine ya kuchetrza mbao na
ujenzi wa banda kwa ajili ya shughuli hizo.
KAMI SEKELUARGA MENGUCAPKAN BANYAK TERIMA KASIH ATAS BANTUANNYA MBAH , NOMOR YANG MBAH BERIKAN/ 4D SGP& HK SAYA DAPAT (350) JUTA ALHAMDULILLAH TEMBUS, SELURUH HUTANG2 SAYA SUDAH SAYA LUNAS DAN KAMI BISAH USAHA LAGI. JIKA ANDA INGIN SEPERTI SAYA HUB MBAH_PURO _085_342_734_904_ terima kasih.
ReplyDeleteKAMI SEKELUARGA MENGUCAPKAN BANYAK TERIMA KASIH ATAS BANTUANNYA MBAH , NOMOR YANG MBAH BERIKAN/ 4D SGP& HK SAYA DAPAT (350) JUTA ALHAMDULILLAH TEMBUS, SELURUH HUTANG2 SAYA SUDAH SAYA LUNAS DAN KAMI BISAH USAHA LAGI. JIKA ANDA INGIN SEPERTI SAYA HUB MBAH_PURO _085_342_734_904_ terima kasih.
KAMI SEKELUARGA MENGUCAPKAN BANYAK TERIMA KASIH ATAS BANTUANNYA MBAH , NOMOR YANG MBAH BERIKAN/ 4D SGP& HK SAYA DAPAT (350) JUTA ALHAMDULILLAH TEMBUS, SELURUH HUTANG2 SAYA SUDAH SAYA LUNAS DAN KAMI BISAH USAHA LAGI. JIKA ANDA INGIN SEPERTI SAYA HUB MBAH_PURO _085_342_734_904_ terima kasih.