Mahojiano
ya moja kwa moja na Mhe. Zitto Zuberi Kabwe katika JamiiForums
,
Kama tulivyoahidi tarehe 19/11/2010 katika Jukwaa la Siasa (katika thread hii), leo tumemkaribisha Mhe. Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia CHADEMA, Zitto Zuberi Kabwe kama mgeni wetu rasmi katika mahojiano ya moja kwa moja.
Tunawashukuru wanachama wote walioshiriki katika kutuma maswali ya kumhoji Mkuu Zitto na pia wale wote waliokuwa wakifuatilia kwa karibu na kusubiri kwa hamu hadi siku ya leo.
Mjadala utaongozwa na AshaDii kwa niaba ya wanachama wa JamiiForums; side comments zitakuwa kwenye Jukwaa la Siasa, hapa - Side comments: Zitto in JF Exclusive Interview on the 22nd of November, 2012
*Kwa wenye access ya kuweza ku-post kwenye forum hii ya Great Thinkers, tunaomba msiingilie mjadala; shiriki kwenye link iliyotolewa ya side comments*
Karibuni

Zitto:
Awali ya yote itoe shukrani zangu za dhati kwa
kupewa fursa hii adimu ya kuhojiwa na wana JF wenzangu.
Nashukuru pia kwa kuwa ni heshima kubwa sana kwangu maana mimi ni mtu wa pili kufanyiwa mahojiano kama haya baada ya kijana mwenzetu Maxence kama 'founder' wa jukwaa letu. Napenda pia ifahamike kuwa mimi ni mmoja wa wanachama waanzilishi wa jukwaa hili na ninafurahi kuona limekuwa na kwa kweli its a force to reckon with.
Zitto ni Mtanzania aliyezaliwa Kigoma, Kijiji cha Mwandiga. Nimekulia katika kitongoji cha Mwanga, nimekwenda shule ya Msingi Kigoma, Sekondari Kigoma, Kibohehe Moshi, Galanos Tanga na Tosamaganga Iringa. Nimepata Elimu ya Juu Chuo Kikuu cha Zanzibar kwa mwaka mmoja, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Uchumi, Scholarship ya InWent Biashara ya kimataifa na Bucerius School of Law and Business Mineral Economics.
Ninaishi Kijijini Kibingo, Kata ya Mwandiga Wilaya ya Kigoma. Pia Tabata wilaya ya Ilala na Dodoma nyakati za Bunge. Ninaishi na mama yangu mzazi na wadogo zangu.

A. Zitto na Ombwe la itikadi
miongoni mwa vyama vya siasa
“ Unalizungumziaje Ombwe la Itikadi Miongoni mwa Vyama vyetu vya Siasa, ambapo tangia mageuzi ya kisiasa na kiuchumi yaingie nchini, ni vigumu kutofautisha itikadi za vyama vya siasa - kinadharia na kivitendo, hasa ukizingitia ukweli kwamba kwa kila chama, sera na itikadi zinazouzwa au kutekelezwa ni za kiliberali, huku wananchi wengi (hasa vijijini) wakiwa hawana ufahamu juu ya madhara na faida ya itikadi hii ni nini.”

- Hii ni changamoto kubwa sana kwa nchi yetu. Itikadi za kisiasa
husaidia kunyoosha sera za vyama. Hivi sasa chama chochote chaweza kuwa na sera
yeyote ile kwa kuwa hakuna uti wa mgongo ambao ni itikadi. Lazima vyama
vijipambanue kwa itikadi zao. Kwa kukosekana kwa itikadi zinazoeleweka vyama
vimekuwa kama 'electoral machines' tu.
Kukosekana kwa itikadi kunafanya vyama kudandia masuala. Mfano juzi hapa
mmesikia Mkutano Mkuu wa CCM umeazimia elimu iwe bure.
CHADEMA tulisema hivi mwaka 2010, CCM wakasema huo ni uwendawazimu kwani haiwezekani. Nakumbuka nilikuwa kwenye mdahalo pale Serena (hivi sasa) mwaka 2010, vijana wa CCM wakaniuliza mtapata wapi pesa za kusomesha watu bure. Nikawajibu kama tuliweza kuwasomesha bure kwa Tumbaku, Kahawa na Pamba, tutawasomesha bure kwa dhahabu, tanzanite nk. Leo CCM wanasema elimu bure. Nimemsikia Lowassa juzi anasema inawezekana. Lowassa huyu nilibishana naye sana mwaka 2010 akisema haiwezekani. Huu ni ukosefu wa itikadi sahihi.
Sababu kubwa pia viongozi wetu hawasomi na hivyo bongo zao hazipo 'sharp' kuweza kuona ni mwelekeo gani wa itikadi wa kufuata. At best tunaimba kama kasuku itikadi zilizoendelezwa nje, hakuna originality.

“Unaiongeleaje sera ya Majimbo
ya CHADEMA?”
- Ni utekelezaji wa kushusha madaraka mikoani,
kupanua uwajibikaji na kuleta maendeleo kwa wananchi. Sera hii ya utawala ndio
suluhisho la masuala mengi ya uwajibikaji hapa nchini. Kuna haja ya kuwa na DC?
Kwa nini wakuu wa mikoa wasichaguliwe na wananchi? Tulipoamua kupendekeza sera
hii kwa wananchi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 tuliambiwa sisi tuna lengo
la kuleta ukabila nchini. Inawezekana kuna maeneo fulani fulani tulikosea
mkakati. Kwa mfano tulianza kusemea suala hili tukiwa mkoani Kilimanjaro, kwa
hiyo CCM ikadakia 'unaona wachaga hawa' sasa wanataka ka nchi kao. Kimkakati
tulikosea.
Tulipaswa kuzindua sera hii kanda ya Ziwa au kanda ya Kusini. Tulijifunza kutokana na makosa haya. Hivi tumejiandaa vizuri zaidi kuielezea sera hii. Tunataka kuimarisha Halmashauri za Wilaya/Miji/Manispaa/Majiji kwa kuoondoa nafasi ya Wakuu wa Wilaya na kada nzima pale Wilayani. Majukumu yote ya kisiasa ya DC atayafanya Mwenyekiti wa Halmashauri. Majukumu yote ya Kiutendaji ya Ofisi ya DC atayafanya Mkurugenzi wa Halmashauri. Wakuu wa mikoa wachaguliwe na Wananchi moja kwa moja na wawe na 'executive powers' kwa mambo ya mkoa husika. Tutayaweka kisheria mambo haya. Hii mambo ya Rais kuteua wakuu wa Mikoa nchi nzima hapana. Watu wachaguliwe.
Ninaamini kabisa kuwa Sera hii ikitekelezwa tutaweza kutumia rasilimali zetu vizuri na mikoa itashindana kimaendeleo badala ya kushindana kwa namna walivyompokea Rais mkoani kwao

Unaona tofauti ya msingi kati
ya CCM na CHADEMA ni IPI?
- CCM imeshindwa kupambana na adui ufisadi,
CHADEMA tunapambana na tutapambana na ufisadi kwa nguvu zetu zote. CCM inaamini
katika soko holela, CHADEMA tunaamini katika soko linalojali. CHADEMA inaamini
katika nguvu ya Umma, CCM inaamini katika nguvu ya Dola.
“Nini kinakuvutia ndani ya CCM
ambacho hakipo CHADEMA?”
Sijakiona bado
“Bado unafikiri wewe kuwa
CHADEMA ni tija kwa jamii kuliko kuwa Chama kingine mfano CCM?”
- Jamii imefaidika sana na kuwa kwangu CHADEMA. Kupitia Bunge na
nje ya Bunge nimeweza kuisimamia Serikali kwenye mengi na hasa masuala ya
rasilimali za Taifa kama madini na kufanikiwa
kupata sharia mpya ambayo imetoa fursa kwa Watanzania kufaidika na utajiri wao
wa madini. Mengi sana
ninayofanya nikiwa CHADEMA nisingethubu kuyafanya ningalikuwa CCM.
“Unalizungumziaje suala la kuwa
na utitiri wa vyama vingi vya siasa vinavyokula pesa za walipa kodi halafu
havina tija wala mchango wowote kijamii zaidi ya kutufilisi, je kuna umuhimu wa
kuifanyia sheria mabadiliko ili kuwe na limitation mfano, vyama vitatu tu?”
Ndio Demokrasia.
Tusiminye kabisa watu kuwa huru kuanzisha vyama vya siasa. Baada ya muda ni vyama vyenye uwezo wa kukonga nyoyo za wananchi ndio vitabakia. Wala hatuna haja ya kuweka sheria. Huko mbele ninaona Tanzania yenye vyama sio zaidi ya 4. Vyama vikubwa 2, CCM and CHADEMA. na CUF watakuwa a balancing party kama ilivyo LibDems UK au Greens and Liberals Ujerumani. Kwa hali ya sasa ya muungano ninaona kuwa CUF yaweza kuwa kama The Bloc Québécois ya kule Canada. Sioni NCCR ikidumu. Soini future ya UDP bila Cheyo na TLP bila Mrema.
Lakini pia kuna uwezekano mkubwa sana wa Kundi moja la CCM kuunda chama kingine cha siasa ambacho kinaweza kuwa na nguvu hata zaidi ya CHADEMA. Baada ya uchaguzi wa mwaka 2015 tutaona hivi new configurations. Tuache watu wawe huru kuunda vyama. Vyenye nguvu vitabakia

B. Zitto na CHADEMA
Nini kipaumbele chako cha sasa kama mwanachama wa CHADEMA?
- Kutumikia chama chetu kwa nafasi nilizonazo.
Natumia nafasi yangu ya Ubunge na Uwaziri kivuli kuhakikisha kuwa chama kinapata taswira chanya mbele ya jamii, Na kinaleta mabadiliko ambayo chama tawala, yaani CCM, kinashindwa kuwafikishia wananchi. Utaona kwamba, kama unafuatilia Bunge, hakuna mkutano wa Bunge unaopita bila hoja mahususi inayojenga taswira chanya ya chama.
Ni bahati mbaya sana kuwa hatutumii baadhi ya mafanikio yetu Bungeni kwenye ulingo wa siasa ma hivyo kuwaacha CCM wanachukua credits.
Kwa mfano, ni kwanini mafanikio ya hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu hatujayafanyia kazi ya kisiasa? Ingawa hatukufanikiwa kumtoa Waziri Mkuu lakini tuliilazimisha Serikali kufanya mabadiliko. Kikwete alisema ni upepo tu, lakini upepo huu ulikuwa na joto kali ukamshinda na tukaacha yeye achukue credit kwa kazi yetu ya uwajibikaji.
Hoja ya juzi ya Mheshimiwa Halima Mdee kuhusu Ardhi inabidi kuifanya ni ajenda ya kisiasa. Hoja ya Mkonge tulikwenda Tanga na ilikuwa na mafanikio makubwa sana. Hoja ya Mabilioni ya Uswiss nayo tunaiachia wanaisemea watu wa CCM kuififiza. Historia inatuonyesha kuwa hoja zote tulizozitumia vizuri nje ya Bunge zilijenga taswira nzuri ya chama ie Buzwagi na EPA.

We ignore this at our own peril
Mkuu, ni kweli kuwa CHADEMA ni
chama cha kidini/kikabila? Na kama ni kweli, tatizo hilo lishughulikiwe vipi? Kama si kweli,
unaweza kuueleza umma wa watanzania una kauli gani juu ya mitizamo hii dhidi ya
chama chenu?
-
Chadema ni chama cha kitaifa. Kingekuwa chama cha kidini au kikabila
kingefutwa. Katika uongozi wa Chadema unapata watu toka mikoa na kabila mbali
mbali, pia watu toka dini mbali mbali. Diversity hii haipatikani katika vyama
vingi humu nchini. Nadhani mtazamo huu unapandikizwa na watu ambao hawakipendi
chama chetu na wanao ona chama kama threat kwa maslahi yao binafsi.
Pia sisi kama chama tunapaswa kuwa makini sana, hasa viongozi tunapofanya kazi zetu ili kutothibitisha taswira hii mbaya dhidi ya chama chetu. Baadhi ya wanachama wa CHADEMA ndio mabingwa wa kueneza jambo hili. CCM nao humo humo wanapandikiza mbegu za chuki. Unakuta Waziri wa CCM anamwita Mbunge wa CHADEMA na kumwambia, fulani bwana mdini sana. Mwangalieni. Kiongozi wa CHADEMA anajiona kapata bonge ya issue na kueneza. Tunachinjwa na CCM kwa upuuzi wetu. Kwa ujinga wetu wenyewe. Chama chetu kimesambaa nchi nzima na viongozi wake ni wa dini zote na makabila yote.

“Mh. Zitto, unaizungumziaje
demokrasia ndani ya chama chako katika chaguzi, teuzi na kupanga safu za
uongozi?”
CHADEMA
ina demokrasia ya aina yake na wanachama tunaridhika nayo. The Party deploys
for or against your wishes and every member must oblige a just deployment. Tuna
utaratibu mzuri sana
wa kujieleza na kutetea hoja zetu ndani ya chama, na baada ya watu wote
kukubaliana tuna hakukusha tunasimama wote kwa kauli moja sehem zote tunapo
wakilisha chama. Sio katika kupanga safu za uongozi tu, ni sehem zote za
uongozi wa chama.
“Kwanini CHADEMA haiwatumii
viongozi wa Mikoa na Wilaya na badala yake inatuma watu toka makao makuu hata
kwa mambo madogo madogo ambayo yangemalizwa na uongozi wa ngazi husika?”
Huo mtazamo unaweza kutokana na kulinganisha
Chadema na vyama vingine. Ieleweke kua Chadema ni chama tofauti na kina utaratibu
wake. Katika chama chetu Viongozi wa mikoa na wa wilaya wana majukumu yao, na makao makuu pia
yana majukumu yake.
Inaweza kutokea mara kwa mara hizi level mbili zishirikiane katika kutekeleza kazi za chama. Hata hivo, tunaendelea kujenga chama kama taasisi, hivyo tunaendelea kujenga uwezo wa viongozi wetu wa mikoa na wilaya ili waweze kumudu majukumu mengi zaidi na kuwaachia wenye kukaa makao makuu kuhusika zaidi na strategies za chama.

“Mh Zitto, unazizungumziaje
harakati za M4C na athari (impact) yake kisiasa na kijamii? Chama kimeweka
taratibu gani nzuri za malezi kwa wanachama wapya wanaojiunga kwenye M4C, kama
bado, huku si kusuka kamba inayoungua?”
Kwa sababu jina lake liko
wazi kabisa, M4C ni moja ya operesheni inayo fanikisha watanzania kujiunga
katika chama huku wakijua kabisa kua malengo ni kuleta mabadiliko chanya.
Impact yake kwa jamii ni kubwa sababu inawaweka wanachama wenyewe kua vyanzo vya mabadiliko. Baada ya kujiunga, ni obvious kua Chama kinatoa mafunzo kwa wanachama wake wapya na hivyo kuwalea kuwa makada wazuri. Hii sio opresheni ya kwanza ya Chama, na haitakua ya mwisho.
M4C sio chama ndani ya chama, M4C ni operesheni ya kujenga chama na kuleta mabadiliko nchini.

Inadaiwa hushiriki kikamilifu
M4C, ni kweli? Nini kauli yako dhidi ya tuhuma hizi?
Ninashiriki sana
kazi za kujenga chama. Nimeshiriki sana
operesheni mbalimbali za chama. Nitaendelea kushiriki nikiwa mwanachama na
kiongozi wa chama.
Halikadhalika wengine tunashughulika zaidi katika kuwakilisha chama Bungeni na mikakati mengine ya kuhimarisha chama, ila tukipata nafasi tunajiunga pia katika kazi za kujenga chama. Mikutano yetu ya chama tunagawana maeneo.
Mimi, kwa mfano kwenye M4C nimepangiwa mkoa wa Manayara na Singida nikiwa na Tundu Lissu na Christina Lissu na Rose Kamili. Mtakumbuka mwanzo mwa mwaka nilifanya ziara Tanga bila viongozi wenzangu. Mtakumbuka nilikwenda Marekani kufungua tawi la chama kule. Nimefanya mikutano Iringa, Hanang nk. Nimeshiriki kampeni za udiwani maeneo mbalimbali nchini. Siwezi kuonekana kila mkoa kila wakati. Pia ninapangiwa kazi.

Je, utaratibu wa kupita mikoani
katika kutafuta nafasi ya kugombea uenyekiti kama ilivyokuwa wakati wa Mbowe
unafaa au CHADEMA irudi katika utaratibu kama
wa CCM?
Hatujawahi
kufanya utaratibu unaosema isipokuwa kwenye Urais mwaka 2005. Hatujarejea tena
utaratibu huo. Mfumo wowote ambao unapanua demokrasia ya chama ni bora zaidi
katika kuimarisha chama. Chama kinakomaa kwa wanachama kushindana kwenye
chaguzi za ndani. Natumai uchaguzi mkuu ujao wa chama utakuwa na wagombea wengi
zaidi ili wanachama wapate uchaguzi wa kweli. Sipendi chaguzi za kupita bila
kupingwa katika chama kinachotaka kujenga demokrasia ya nchi.
Mheshimiwa Zitto
Viongozi/CHADEMA imekuwa mstari wa mbele kufichua ufisadi. Kuna taarifa kuwa
kuna mwanachama wenu katafuna fedha za M4C, ni kweli? Kama ni kweli,
ameshughulikiwaje? Kama hajashughulikiwa, ni kwanini mko kimya?
Nasikia
suala hili hapa, tupeni ushahidi na tutachukua hatua mara moja.
Zitto wewe ni naibu katibu mkuu
wa CHADEMA, Mara nyingi matamko ya chama yametolewa na Katibu, Mwenyekiti,
Mnyika (tangu kabla hajawa msemaji) na mara chache wanasheria km Lissu, Marando
na Prof.Safari. Kwanini Zitto umekuwa mbali sana
na matamko haya ya CHADEMA ukiwa kama Naibu
Katibu mkuu? (Naamini hutojibu ni mgawanyo wa kazi)
Naibu
Katibu Mkuu sio msemaji wa chama. Katika kujibu suala la demokrasia katika
chama nilisema kuwa kuna utaratibu wa kujadili hoja mbali mbali ndani kwa
ndani, yakiwemo matamko ya chama.
Katibu mkuu wa CHADEMA anapotoa matamko ya chama anatoa yale yaliyojadiliwa na wanachama wote, nikiwemo mimi, hivyo kuwakilisha maoni yangu pia. Sidhani kama kuna umuhimu wa kuifanya kazi hiyo wakati nimeridhika kua maoni yangu yanawakilishwa kupitia utaratibu wa chama.

Unafikiri CHADEMA uliyoikuta
mwanzo ndiyo hii ya sasa au kuna mabadiliko? Kama kuna mabadiliko ni yepi na
unafanya nini kufanya CHADEMA iwe kama ambavyo
ulitaka iwe?
CHADEMA
ni chama kinachokua kwa kasi sana,
na kadiri kinavyokua kinabadilika positively. Moja ya mabadiliko hayo ni idadi
ya wanachama, nyingine ni kuweza kushika Uongozi wa Upinzani Bungeni, nafasi
ambayo ilikua ya CUF nilipo ingia chama. Chama hivi sasa kipo kila
mahala.
Nakumbuka mwaka 2005 tulikwenda Mafinga kuhutubia tukapata watu 20 tu kwenye mkutano. Leo tunaombwa kwenda huko. Chama kina influence maamuzi ya nchi hivi sasa. Hayo yote ni mabadiliko makubwa na mazuri, na ninafurahi kuwa sehemu ya mafanikio ya chama changu.

Unafikiri namna CHADEMA
inavyoendesha siasa zake kuna uwezekano wa kushika dola mapema (2015)? Kama
ndiyo kwanini na kama hapana unafikiri
mabadiliko gani yanatakiwa kufanyika kuelekea 2015?
Sina mashaka na hili. Nitafafanua zaidi baadaye
CCM wanadai kuwa nyinyi CHADEMA
hamna presidential materials, una kauli gani juu ya hili?
Kweli
unategemea kuwa chama tawala kinaweza kukisifu chama cha upinzani kwa kuwa na
presidential material? Mimi ni Presidential material kwa mfano.
Nina Uwezo, Uadilifu na Uzalendo wa kuweza kuwa Amiri Jeshi Mkuu. Dkt. Slaa ni Presidential Material. Mbowe ni Presidential material. Kitila Mkumbo ni Presidential material. Wapo wengi sana ndani ya CHADEMA wenye sifa za kuwa Marais. Sina mashaka kabisa hilo.

Una muono gani kuhusu upinzani
nchini na nini nafasi ya upinzani hasa CHADEMA kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka
2015 ukilinganisha na chama tawala CCM?
Ili Tanzania iwe salama ni lazima CCM
ishindwe uchaguzi. CCM ikishinda tena mwaka 2015 itavunja sana moyo wa wananchi na wengine wanaweza
kukata tama. Lakini pia CCM imechoka na haina nguvu za kutosha kukabiliana na
changamoto za nchi hivi sasa.
Njia pekee ya kuisadia CCM iweze kujipanga upya ni yenyewe kondoka madarakani. CHADEMA ina nafasi kubwa sana ya kushinda na kuongoza dola. Muhimu chama kijipange na kuonekana kama chama kilichotayari kushika dola. Tuyatende tunayoyasema na tujiimarishe zaidi.

C.
Zitto na kuhusishwa na CCM
Kumekuwa na shutuma za mara kwa
mara kuwa una ukaribu uliokithiri na Chama kuu pinzani kwa CHADEMA yaani CCM.
Unasemaje kuhusiana na tuhuma hizo?
Ukitaka kummaliza mwanasiasa yeyote wa upinzani
hapa Tanzania
mhusishe na ama usalama wa Taifa au CCM. Ndivyo ilivyokuwa kwa Mabere Marando
miaka ya Tisini. Marando ameishi kuweka sawa historia ingawa propaganda dhidi
yake zilikuwa kali sana
kiasi cha kuogopwa kweli kweli. Napita njia hiyo hiyo ya Marando na wanaonipaka
matope haya wataona aibu sana
ukweli utakapodhihiri.
Siku za mwisho za uhai wake ndugu Chacha Wangwe naye aliambiwa ni CCM na kwa kweli alikufa akiwa na chuki sana kuhusu tuhuma hii.
Faida kubwa niliyonayo mimi ni kwamba, mtaji wangu wa kisiasa ulikuwa ni mkubwa mno na ndio maana tuhuma hizi hazijaniathiri. Ninaamini tuhuma kama hizi zingekuwa kwa watu wengine wangekuwa wameshafutika kwenye historia ya siasa. Sijawahi kuwa mwanaCCM, familia yangu yote kabisa ni waanzilishi wa CHADEMA. Sina historia na CCM. Inawezekana wanaosema mimi ni CCM wengi wao wamewahi kuwa CCM, wana familia zao ndani ya CCM na wamewahi kula matunda ya CCM. Mimi sijawahi na wala sitawahi.

Inasemekana kua ukaribu huo
unaweza kuonekana kupitia ukaribu wako na Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni rais
wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. Unasemaje hapa?
Kuhusu
Rais Kikwete, kwanza ifahamike Jakaya Kikwete na Zitto Kabwe wana mahusiano yao nje ya siasa na hata
siku moja hatujadili vyama vyetu. Rais Kikwete anaamini katika uzalendo wangu.
Mimi ninamheshimu Rais Kikwete kama Mzee wangu. Kuita sisi ni marafiki is understatement, yeye ni mzee wangu. Tunaheshimiana, lakini ninaiheshimu zaidi Tanzania na ninaipenda zaidi Tanzania. Kama inavyoonekana, kazi zangu zinajihidhirisha Bungeni kwamba ni mmoja wa wabunge ninayeisumbua sana Serikali yake. Kutokana na hoja zangu nimemlazimisha kufanya mambo kinyume na mipango yao. Leo tuna sheria mpya ya Madini kwa sababu ya hoja ya Buzwagi. Ninafurahi sasa mgodi wa TanzaniteOne hisa asilimia 50 zinachukuliwa na Watanzania kutokana na mapendekezo yangu mahususi kwamba vito vya thamani, mgeni asiwe na zaidi ya asilimia 50.
Mwaka huu nimemlazimisha kupangua baraza la mawaziri kufuatia hoja yangu ya kutokuwa na imani na waziri mkuu iliyoungwa mkono na wabunge wengi bila kujali vyama. Hebu niambie kama ningeweza kupata mafanikio kama haya dhidi ya Serikali ya mtu mnayesema rafiki yangu. Wengine watasema, aah JK huwa anamtuma kufanya haya. Iwe jua au mvua ni lawama tu. Lakini maisha ya kisiasa haya. Yana mwisho, Rashidi wa KULI alisema.

Mkuu, vipi kuhusu kuonekana
kwako in public pamoja na rais sehemu tofauti hadi safari za nje ya nchi.
Suala la kusafiri na Rais ni suala la kawaida sana. Nashangaa sana namna linavyokuzwa
wakati ni wazi kabisa kua Rais lazima asafiri na wabunge, na anae wateua
wabunge ni Spika wa Bunge. Kila Rais, Makamu wa Rais au Waziri mkuu wanapo
safiri huambatana na wabunge wa kambi zote mbili.
Kwa kuweka rekodi sawa Rais amesha safiri na wabunge wafuatao wa Chadema: Christina Lissu (Australia), Chiku Abwao (Burundi), Grace Kiweli (Scandinavia), Lucie Owenya (US), nk. Makamu wa Rais kesha safiri na Ezekiah Wenje (Uturuki) na Esther Matiko (Uturuki) Waziri Mkuu pia kesha safiri na wabunge wa Chadema.
Toka nimekuwa mbunge nimesafiri na Rais mara mbili tu: Mara ya kwanza ilikua sherehe za uhuru za Sudan Kusini. Nilikwenda kwa taratibu hizo za Bunge. Mara ya pili ni Ethiopia, Kumzika Meles Zenawi. Hii niliomba mwenyewe kwani nilipenda kwenda kumzika mwanasiasa huyu niliekuwa namheshimu sana barani Afrika.

Inasemekana kuwa ni Kwa sababu
yako ndio maana rais JK hakumnadi mgombea wa ubunge wa CCM wa jimbo lako katika
uchaguzi mkuu uliopita na kwamba ndio maana hukushiriki katika kuungana na
wanachama wako katika kumsusia JK siku ile anafungia bunge.
Rais Kikwete hakufika jimboni kwangu kumnadi
mgombea wa chama chake. Napenda niwakumbushe, sio mwaka 2010 tu, toka nimekuwa
mbunge Rais Kikwete hajawahi kuja kwenye kampeni jimboni kwangu. Hakuna
makubaliano yeyote, bali anaheshimu mchango wangu kwenye nchi yangu. Mwaka 2005
hakuja Kigoma Kaskazini. Mwaka 2010 hakuja Kigoma Kaskazini. Lipumba pia hakuja
Kigoma Kaskazini kunadi mgombea wake wa CUF.
Mwaka 2005 katika Jimbo la Musoma Mjini, aliyekuwa mgombea Urais CHADEMA ndugu Mbowe, hakumnadi mgombea wa CHADEMA bali alimnadi mgombea wa CUF. Mwaka 2010 Slaa alipofika Kyela alimnadi mgombea wa CCM dkt Mwakyembe. Kama ilivyo kwa wengine wenye maamuzi ya kuthamini kazi za wagombea wa vyama vingine, Rais Kikwete naye anayo haki ya kuheshimu na kuthamini kazi zangu katika nchi yetu. Mwakyembe yupo kwenye majukwaa ya CCM licha ya kwamba alinadiwa na Mgombea Urais wa CHADEMA.

Vipi madai kuwa unatumwa na CCM
ili kupunguza nguvu ya CHADEMA? Kama si kweli unadhani kwanini watu wanakuona kama pandikizi ndani ya CHADEMA?
Baadhi ya watu wanapandikiza chuki hizi kwa
sababu zao wenyewe. Hawanisumbui maana najua ni kikundi kidogo cha watu
wachache wenye malengo yao
ovu. Wajue tu kwamba hawawezi kuwadanganya Watanzania ambao wanafanya maamuzi yao sio tokana na
propaganda ila kutokana na matendo ya kila mmoja.
Onyo: Watu hao hawawezi kummaliza Zitto kisiasa bila kuiathiri CHADEMA maana the imaage of Zitto is so intimately intertwined with CHADEMA that you couldn’t attack Zitto without jeopardizing the image of Chadema, and vice versa.
Wanaoeneza sumu hii hawana nia njema wala mapenzi na CHADEMA. Hawaelewi siasa. Wanafurahisha maadui wa CHADEMA. Maadui wanawachochea kwa kuwapa habari za uwongo na wao wanadhani watammaliza Zitto. Huwezi kummaliza Zitto bila kuiathiri CHADEMA. Hawatafanikiwa.

Ni kweli kuwa una mkakati wa
kuhamia CCM kabla ya 2015?
Sijawahi
wala kufikiria kuhamia CCM. Kama nilivyosema
hapo awali, sijawahi kuwa mwanachama wa chama kingine chochote tofauti na
CHADEMA. Namwomba mungu kuwa niondoke duniani nikiwa chama hiki hiki. Siamini
katika kuhama vyama. Ninaamini katika mfumo imara wa vyama vingi nchini.
Ninaamini katika demokrasia pana.
Vipi tetesi kuwa wewe na
Kafulila mmeanzisha chama na una mkakati wa kutimkia huko?
Swali hili na lililotangulia yanaonyesha kuwa
hizi kweli ni tetesi tu. Sasa kama unasema nina mkakati wa kuhamia CCM. Tena
kuna tetesi nimeanzisha chama na nataka kuhamia huko, sasa mimi nina vyama
vingapi nitakavyohamia. Sijawahi hata kufikiria kuanzisha chama cha siasa.
Chama changu ni CHADEMA na sitaondoka CHADEMA. Kinachonisikitisha ni kwamba
kuna viongozi wa CHADEMA wamekula sumu hii na bila woga wanaisema kana kwamba
ni kweli.
It is very unfortunate Kiongozi wa chama makini kama CHADEMA kuamini ujinga na kuingia kwenye mitego kama hii. Nataka ijulikane wazi kabisa kwamba, CCM haitachoka kutugawa. Haitachoka kupandikiza chuki miongoni mwetu. Wameshajua udhaifu upo wapi na wahenga walisema kamba hukatikia?

D.
Zitto na Kigoma
Unaweza orodhesha utofauti wa
Kigoma ya sasa na Kigoma kabla ya Zitto kuwa mbunge wake?
Hili
watasema watu wa Kigoma wenyewe. Sio watu wa jimboni kwangu tu bali watu wa
mkoa mzima wa Kigoma. Kigoma ya mwaka 2005 na Kigoma ya mwaka 2012 ni sawa na
kichuguu na mlima Kilimanjaro. Tunaendelea kusukuma maendeleo zaidi ya Mkoa
huu. Nafurahi sana
kuwa sehemu ya mabadiliko haya ya mkoa wangu. I am very proud.
Hata hivo naamini bado kuna mengi zaidi yanayo takiwa kufanyika na nitashirikiana na wabunge wetu watakao kuja kuhakikisha Kigoma inasonga mbele. Ni vema watu wa Kigoma watoe hukumu yao wao wenyewe badala ya mimi kuanza kubrag hapa. Watasema barabara zilikuwaje na sasa zipoje. Watasema hali ya umeme. Watasema hali ya kilimo cha kahawa. Watasema hali ya elimu na afya. Humu kuna watu wa Kigoma, waseme wenyewe!

Mkoa wa Kigoma
unanufaika/utanufaikaje na ukaribu wako na serikali ya Ujerumani?
Sina
ukaribu na Serikali ya Ujerumani.
Umeandaa mikakati gani
kuhakikisha Chadema inatetea vema hicho kiti chake?
CHADEMA ni chama imara sana Kigoma Kaskazini. Kina mtandao kila
kitongoji na kina viongozi mahiri kwenye vijiji. Tunachohitaji ni kupata
mgombea mzuri.
Napenda niseme hapa kwa uwazi kabisa. Viti vyote walivyoshinda NCCR Kigoma isipokuwa Kimoja vilichukuliwa na vijana waliokuwa CHADEMA. Kwanini walitoka ni jambo ambalo sote twapaswa kutafakari (wana chadema) maana naona kuna watu wanatoa majibu mepesi sana kuhusu suala hili. Wengine wanadiriki kusema niliwasadia vijana hawa. Sikuwasaidia lakini nilikataa kwenda kufanya kampeni dhidi yao maana matokeo yake ingekuwa ni CCM kushinda kwa sisi wapinzani kugawa kura.
Kuna wenzangu wangependa bora CCM ishinde kuliko mtu kama Kafulila kushinda, nilikataa nadharia hiyo. Hivi sasa Kigoma ina wabunge wa upinzani 5 kati ya majimbo 8. Wabunge 4 kati ya hao ni wana CHADEMA by nature lakini kushindwa kwetu kuvumulia tofauti zetu kumefanya kuwapa NCCR viti. Ukiangalia kura za Urais Kigoma ilipata asilimia 45 ya kura zote na hata kushinda kwenye baadhi ya majimbo. Lakini tulipata kiti kimoja tu tena kwa mbinde sana. Hili ni somo. Tukijifunza tutashinda viti vyote vya mkoa wa Kigoma bila shida yeyote ile.

Kuna mtu ambaye umemuandaa
kugombea nafasi ya Ubunge Kigoma Kaskazini? Ni kwa tiketi ya chama gani? Kama yupo tunaweza mfahamu au bado ni siri kwa sasa? Vipi
ndugu Yared Fubusa ana nafasi gani kuelekea 2015?
Sijaandaa mtu. Nachukia siasa za kuandaa watu.
Mimi sikuandaliwa kugombea Kigoma Kaskazini. Nilitaka kuwa Mbunge na nikaomba
ridhaa. Yeyote anayetaka kuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini lazima aanze sasa kushiriki
kazi za chama chetu, tumjue na tumpime na wengine kasha Mkutano Mkuu wa chama
katika Jimbo utateua mmoja aliyebora kabisa.
Yared Fubusa ni kijana mzuri sana mwenye maono na mwenye mapenzi ya dhati ya Kijiji chake cha Kiganza na Kata yetu ya Mwandiga na mkoa wa Kigoma. Ninamshauri aanze sasa kushiriki katika kazi za chama chetu cha CHADEMA ili wanachama wamjue na wampime. Anaweza kuwa Mbunge mzuri sana. Nitafurahi kama nitapata mtu wa aina yake kuendeleza jimbo letu. Yeyote anayetaka Ubunge Kigoma Kaskazini ajitokeze sasa. Mimi sitaandaa mtu yeyote. Nataka, kama mpiga kura, tupate mtu safi.

Mgodi wa chumvi wa Uvinza
uliouzwa kwa bei ya hisani kwanini hawalipii yale maji ya chumvi ambayo yapo
ardhini toka kugunduliwa kwake miaka ya 1800's ("Brine") kwa kutumia
"flow meter" kama mwananchi wa kawaida wa Kigoma Mjini ambaye
analipia maji ya KUWASA kutoka ziwa Tanganyika? Je, wawakezaji hao
waliuziwa hata mkondo wa maji ya chumvi yaliyopo ardhini wakati wao hawakuwa
wagunduzi?
Nitafuatilia suala kwenye kamati yangu. Sikuwa
nimelitilia maanani.
Pamoja na kuuziwa kiwanda hicho
kwa bei ya hisani, kwanini bado wanaendelea kutumia nishati ya kuni kutoka
kwenye miti asili ambayo hawakupanda wao badala ya kutumia nishati mbadala?
Ndugu Kafulila anafuatilia suala hili kwa kina sana. Kuna kazi
inaendelea hivi sasa kuhusu suala hili sipendi tuiseme hadharani.
Katika vipindi vyote hivi vya
ungozi wako wananchi wa Kigoma Kaskazini ungependa wakukumbuke kwa lipi?
Ufahari wa Utu wao. Leo watu wa Kigoma hawaoni
aibu kujitambulisha hivyo. Haikuwa hivyo miaka ya nyuma. Hili ni kubwa sana kwangu kuliko mamia
ya kilometa za barabara au makumi ya megawati za umeme au Uwanja wa ndege wa
Kimataifa.
E.
Zitto na Maoni juu ya Tanzania
Nini ni Dira ya Kabwe Zuberi
Zitto kwa Tanzania?
Tanzania ambayo kila Mtu ana fursa sawa ya kujiendeleza na kuliendeleza Taifa
bila vikwazo vyovyote. Tanzania
yenye heshima mbele ya Mataifa ya dunia, wenye watu wanao thamini Utu wa
binadam wote duniani, yenye watu werevu wanao tambulika nyumbani na kimataifa,
na wenye siha njema. Mwono chanya kuhusu nchi yao na majirani wao. Napenda kuona Taifa
imara na bora barani Afrika. Taifa lisilo na taswira ya ufisadi. Taifa la
kujivunia. Inawezekana.
Kama leo ungechaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania
chini ya katiba ya sasa ukiwa amekuta maadui wale watatu (ujinga, umaskini
na maradhi) wakineemeka hasa wakiwa wamepata mwenzao ufisadi, ungetumia
jeshi gani/mbinu gani kupambana na maadui hawa?
Kwanza kuibadili Katiba hiyo ingekuwa suala la kwanza maana huwezi kupambana
na ufisadi kwenye Katiba ambayo ni mbaya.
Pili ningeimarisha sana miiko ya uongozi na kuweka bayana kwamba yeyote anayetaka uongozi wa Umma atumikie umma, biashara aweke pembeni. Hata nchi zilizoendelea zinafanya hivi (conflict of interest code). Hii ndio inaimarisha ufisadi.
Tatu, uwazi wa mali za viongozi, uwazi wa mikataba yote ya kunyonya rasilimali na uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi.
Ukishaweka misingi hii na hasa misingi ya uwazi na uwajibikaji kazi ya kupambana na rushwa inakuwa rahisi sana. Hivi sasa tunashindwa kwa sababu hao wanaopaswa kupambana na rushwa wao wenyewe wana maslahi na wanazuia mabadiliko. I am anti status quo person all my life and we need just that.
Suala la mgongano wa maslahi nimeliandikia mara kadhaa na hata jana kuna makala kwenye RaiaMwema kuhusu suala hili. Pia niliandika muswada binafsi Bungeni kuhusu suala hili na niliuweka hapa JF napia kwenye blog yangu zittokabwe.com. Hili ni suala linahitaji sana msukumo ni kuondoa ufisadi nchini.

Kwanini Tanzania ni
Maskini? Mkakati gani wa anaouona kuwa unaweza kutambua vipaumbele vya
kuondokana na umasikini wa Tanzania?
Tanzania ni masikini kwa sababu viongozi wetu wamechagua tuwe masikini. Njia
moja kubwa na ilio endelevu ya kutokomeza umasikini Tanzania
ni kuwekeza walipo Watanzania wengi na kuwapa fursa za ajira na ujira, fursa za
kuzalisha utajiri kwa kuongeza uzalishaji mali.
Umasikini wa Tanzania utaondoka kwa kuwa na Maendeleo Vijijini. Ili kupata rasilimali za kuwekeza vijijini ni lazima kuondokana na upotevu mkubwa wa rasilimali za nchi kutokana na matumizi mabaya (kama posho), ufisadi, wizi na udokozi, pia kuzuia ukwepaji mkubwa wa kodi. Kazi ndio kipimo cha Utu itakuwa ni kauli mbiu muhimu ili kurejesha ‘attitude’ ya kufanya kazi badala ya kuwa Taifa la wanyemelea-kipato (rent-seekers).

Kama kijana, umetembea nchi
kadhaa duniani, kwa muono wako ni wapi wananchi, viongozi, serikali na taifa
kwa pamoja tunakosea katika kulisongesha gurudumu la maendeleo Tanzania?
Hatuna wivu wa maendeleo. Tumekata tamaa. Hatuna
‘ambition’ za kuacha legacy kama walivyo kina
Mahathir, kina Meles nk. Hatuna attitude ya maendeleo. Watu wenye madaraka
hawana mawazo mapana, hawaoni mbali., na hawana constancy and consistency
katika strategies zao za kuendesha nchi. Ukienda kwenye blog yangu soma a post
imagine Tanzania
utaona potential ya nchi hii.
Ikiwa ndani ya uwezo wako i.e
tuchukulie umepata urais; ni njia gani ambayo unaweza kutumia kufuta na
kumaliza Udini ambao unaanza kujidhihirisha kwenye siasa za Tanzania?
Udini ni state of mind. Tatizo Tanzania
tumekuwa kwenye state of denial.
Malalamiko ya Udini katika nchi yameanza siku nyingi sana. Njia ni moja tu, Serikali kutoshughulika na masuala ya Dini na viongozi wa dini kutojiingiza kwenye siasa za vyama bila kupoka uhuru wao wa mawazo au wa kujiunga na vyama vya siasa. Ukiwa na Serikali inayotenda haki kwa watu wote bila kujali wana Sali au wanaSwali hapatakuwa na malalamiko haya.
Hii sio mara ya kwanza tunaona vurugu za kidini kwenye nchi. Kwani mmesahau suala la maduka ya nguruwe miaka ya tisini? Mmesahau suala la mwembechai la miaka hiyo hiyo? Mmesahau mauaji ya Arumeru? Muhimu ni Serikali kuwa imara kuhakikisha tunapiga vita ‘chuki’ kisheria na kutenda haki kwa watu wote bila kujali dini zao. Udini ulivyo sasa ni kansa inayotutafuna kidogo kidogo. Nimeshuhudia mwenyewe udini mkali sana wakati wa kampeni mwaka jana Jimboni kwangu ulioendeshwa na dini zote kuu - Waislam na Wakristo kila mmoja kwa mwono wake.
Nimesoma jana makala ya MwanaKijiji kuhusu namna ya kushughulika na suala hili. Kuna haja ya kuzungumza kwa uwazi bila jazba suala hili. Ningekuwa ni Rais leo ningeunda Tume ya Ukweli na Maridhiano kujadili kwa uwazi na mapana yake suala la Udini. Tusipochukua hatua nchi hii itapasuka vipande. Haya mambo ya Gesi na Mafuta haya ndio yatatumika na maadui wa nchi yetu kutugawa.
Tuwe Makini sana. Tusione tu hizi vurugu kwa juu juu. Tuzungumze

F.
Zitto na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Tukiachana na hoja juu ya
umuhimu wa wananchi wenyewe kuamua, je, wewe binafsi kama mmoja ya hao
wananchi, unadhani mfumo upi ni bora ambao utaweza kusaidia pande zote mbili
kuhisi zinafaidika na muungano?
Kwanza kabisa niweke wazi kwamba mimi ni muumini
wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Shirikisho la Afrika Mashariki na
Mwanamajui wa Afrika (Pan Africanist). Lazima tuulinde muungano wetu kwa
kuufanyia marekebisho makubwa sana ikiwemo kutoa uhuru mpana kwa pande za
Muungano kufanya mambo yao. Muungano wenye Zanzibar na Tanganyika zenye Mamlaka
ya kutosha (Kina ndugu Jussa wanasema Mamlaka kamili, ukisema mamlaka kamili ni
sawa na kusema hakuna muungano). Baada ya utangulizi huu, ningependa muungano
uwe na muundo gani?
Muundo wa Muungano uwe wa Nchi moja, Dola moja, Taifa moja. Serikali tatu. Kuwe na Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye ni Mkuu wa nchi na Mtendaji kwenye masuala ya Muungano tu ambayo yatakuwa machache kama Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Sarafu, Sera za Fedha, Biashara ya Kimataifa, Kodi za kimataifa, usimamizi wa Rasilimali za Taifa, Uraia nk. Zanzibar watakuwa na Waziri Mkuu Mtendaji na Tanganyika hivyo hivyo. Chama chenye Wawakilishi wengi kwenye Baraza la Wawakilishi la Tanganyika kitatoa Waziri Mkuu na kuunda Serikali na Zanzibar hivyo hivyo. Bunge la Muungano litachagua wajumbe wake kutoka kwenye kila mkoa wa Tanzania wajumbe wawili. Maamuzi yataamuliwa kwa zaidi ya nusu ya kura kwa Wabunge kutoka kila upande wa Muungano.

Kwa mtazamo wako kama Zitto, Je
unadhani kuna mambo gani yaliyomo ndani ya Azimio la Arusha ambayo bado
yanaweza kutusaidia katika kipindi hiki kigumu bila ya kujali itikadi za
kisiasa?
- Miiko
ya Uongozi.
- Serikali kuwa msimamizi mkuu wa maendeleo ya nchi badala ya kuachia soko kila kitu.
- Msisitizo wa maendeleo vijijini.
- Serikali kuwa msimamizi mkuu wa maendeleo ya nchi badala ya kuachia soko kila kitu.
- Msisitizo wa maendeleo vijijini.
Kuna lingine la muhimu katika
hili mkuu… Wengi wanaliponda Azimio La Arusha lakini ni mabingwa wa kukimbia
kujadili kitu mbadala wa Azimio la Arusha; Wakibanwa, wanakimbilia Katiba Mpya;
Hivi ni vitu viwili tofauti; Declarations mbalimbali ni muhimu sana kwa taifa
katika kujipanga kimaendeleo. Unadhani kwanini?
-Katiba sio mwarobaini wa matatizo ya nchi yetu.
Unaweza kuwa na Katiba nzuri sana lakini fukara tu. Maazimio yanatoa mwelekeo
wa nchi kutokana na nyakati. Katiba inaweka tu misingi ya mtajiongoza namna
gani na kwa mipaka gani na maono. Azimio kama ilivyo Azimio la Arusha linaweka
utaratibu wa kutekeleza katiba
H:
Zitto na KATIBA Mpya
Unazungumzia vipi suala la
majina wajumbe wa kamati ya kukusanya maoni ya katiba mpya kuchaguliwa na rais?
- Hili halina mjadala tena maana tume imeshaundwa
na majina yameshatangazwa. Vyama vilipeleka majina kwa Rais na Rais akateua
kutokana na orodha ambayo yama vimepeleka. Hili swali halina tija kwa sasa.
Ni kipengele/vipengele gani
katika katiba ya sasa vina mapungufu makubwa zaidi kuliko vingine na una maoni
gani?
Katiba nzima ina mapungufu na hivyo tunaandika
upya kabisa. Katiba itakayo tufaa ni yenye kulinda maslahi ya taifa, sio vyama
au watu binafsi. Katiba hiyo inatakiwa kuweka msingi ya Tanzania tunayo itaka.
Napenda Katiba ambayo itaimarisha sana Uwajibikaji. Kama Katiba ingekuwa ni neno moja tu basi mimi ningechagua neno hilo liwe 'UWAJIBIKAJI' yaani Accountability. Huu ndio msingi wa Taifa kwa wananchi kuwa na uwezo wa kuwawajibisha viongozi na viongozi kuwajibika kwa wananchi.
Ningependa kuona Katiba ambayo inaweka maliasili zote za nchi, zilizopo chini ya ardhi na juu ya Ardhi chini ya mamlaka ya Dola. Katiba Itamke kuwa Madini, Mafuta, Gesi Asilia, Ardhi na vilivyomo ni mali ya nchi na Katiba na Sheria itaweka utaratibu wa kuendeleza rasilimali hizo kwa faida ya wananchi wote.
Ningependa kuona Katiba ambayo inatupa matumaini ya Taifa tunalojenga. Katiba itakayotumikia wananchi na sio wananchi kutumikia katiba.
Napenda kuona katiba itakayoimarisha Utu wa Mtanzania. Katiba itakayoweka misingi ya dhati ya Utu, Uzalendo na Uadilifu wa wananchi kwa Taifa lao na wa viongozi kwa wananchi.

Unakubaliana na dhana ya kuwa
Spika wa bunge amekuwa na madaraka makubwa mno hivyo kuna umuhimu wa kupunguza
baadhi ya madaraka.
- Spika hana madaraka yoyote. Unaposema madaraka
makubwa mno maana yake nini? Kazi ya Spika ni kusimamia mijadala tu Bungeni.
Spika sio mtendaji wa Bunge. Jambo la msingi ni kuboresha kanuni za Bunge ili
ziweze kuweka uhuru mkubwa zaidi wa mawazo ndani ya Bunge.
Mkuu Zitto, ningependa kujua
kitu kingine kutoka kwako. Katika Mabadiliko ya Katiba yanayokuja kuna
uwezekano mkubwa wa MAWAZIRI wasitokane na nafasi za UBUNGE. Kwa muono mwingine
wewe umetangaza kutogombea ubunge jimboni kwako. Hii inaweza kuchukuliwa kuwa
unawinda UWAZIRI kwa kulifikiria hili?
Duh, umewaza mbali hata mimi sikuwa nimewaza
hivyo. CHADEMA ikishinda niwe au nisiwe Mbunge ninaamini nitakuwa Waziri ili
kuweza kutekeleza mabadiliko tunayohubiri katika harakati.
Nimetangaza kutogombea Ubunge, kwanza kuomba ridhaa ya chama changu kuwa mgombea Urais na hilo lisipowezekana nitakuwa mpiga debe wa mgombea Urais. Sitaki itokee tena yaliyotokea mwaka 2010 ambapo mgombea Urais alibaki mpweke kwani kila mtu alikwenda kugombea Ubunge.

Je, utaratibu wa sasa wa bunge
la JMT wa kupiga kura kwa kuuliza wanaosema NDIYO na wanaosema SIYO ni sawa na
unakidhi matwaka ya kidemokrasia uendelee au ubadilishwe? Kwanini?
Kuna mashine ya ki elektroniki za kupiga kura
ndani ya Bunge. Nadhani tuanze kutumia hizo ili pia kuweka rekodi za wabunge
kuhusu kura zao. Itasaidia sana kujua misimoa ya watu kwenye masuala mbalimbali
ya nchi.
I:
VITI MAALUM:
Nini msimamo wako juu ya uwepo
wa wabunge zaidi ya 100 wa viti maalum ambao kimsingi wanaligharimu taifa
mamilioni ya fedha?
Naunga mkono mfumo wa uchaguzi utakaohakikisha
kuwa vyombo vya maamuzi vinakuwa na uwiano sawia wa wanawake na wanaume.
Napinga mfumo wowote wa upendeleo maana inadhalilisha.
Hivyo Katiba mpya ifute mfumo wa viti maalumu na kuweka mfumo wa uchaguzi utakaohakikisha vyombo vya maamuzi vinakuwa na wanawake na wanaume kwa uwiano sawia. Mimi ni muumini wa mfumo wa Uwakilishi wa uwiano (Proportional Representation).
Nchi za scandinavia zina mfumo mzuri sana wa uwiano ambapo viti vya Bunge vinapatikana kutokana na uwiano wa kura ambazo kila chama kimepata. Sio lazima tufuate mfumo wao, tunaweza kuwa na mfumo mchanyato. Ujerumani wanafuata mfumo mchanyato na kuna wabunge wengi tu wanawake.
Rwanda pia imefanikiwa kuwa na wanawake wengi sana Bungeni ingawa inabidi kuwa makini kufuata mfumo wa Rwanda demokrasia yao ina mashaka kidogo. Hata hivyo kuja jambo la kujifunza.

J:
Zitto na matumizi ya vyombo vya usalama wa taifa katika kulinda maslahi ya
chama tawala
Kuna taarifa kuwa CCM inatumia
vyombo vya ulinzi na usalama katika kuudhoofisha harakati za vyama vya
upinzani, na hasa CHADEMA. Mheshimwa Zitto, una mtizamo gani katika hili?
Ni kweli kabisa. CCM inatumia sana vyombo vya
dola kumaliza upinzani. Hata hii ya kugawa wanachama na kupakaza matope baadhi
ya viongozi ni kazi ya usalama wa Taifa. Wanapandikiza chuki ili viongozi
tusiaminiane. Viongozi vichwa maji wasiojua kazi ya usalama wa Taifa
wanafurahia mambo haya kumbe wanatumika
Mhe, kuelekea uchaguzi wa mwaka
2010 gazeti la MwanaHalisi lilichapisha mawasiliano ya simu baina yako na ndg
Jack Zoka wa TISS, mpaka leo sijasikia sehemu ukikanusha; kwakuwa hakuna
kanusho toka kwako, unaweza kutueleza mazungumzo yenu yalihusu nini?
Naomba nikusahihishe kwamba MwanaHalisi
walichapisha mawasiliano hayo baada ya uchaguzi. Suala hili nimeshalisemea sana.
Kwanza ni kweli mimi ninawasiliana na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama wakiwemo TISS, Polisi, TAKUKURU na hata JWTZ. Kama kuna kiongozi yeyote wa nafasi kama yangu ambaye hafanyi mawasiliano na watumishi hawa wa Umma basi kiongozi huyo hafai kuwa Kiongozi.
I challenge mtu yeyote aseme kama kuna kiongozi yeyote wa vyama vya siasa ambaye hafanyi mazungumzo na watu wa usalama nk. Jambo la msingi ni mazungumzo mnayoyafanya yanahusu nini? Yanahujumu chama? Niliwaambia viongozi wangu wa chama kwenye vikao vya chama kuwa, kama kuna chembe ya hujuma kwa chama kwenye mazungumzo yangu na watu kama Zoka basi nitaachia nafasi zangu zote uongozi kwenye chama na Ubunge. Nikawaambia wale waliosema wanao ushahidi wa mazungumzo hayo wayaweke wazi. Sio MwanaHalisi wala washirika wa MwanaHalisi waliofanya hivyo.
MwanaHalisi ilikuwa inafanya kazi ya siasa za ndani ya chama. MwanaHalisi walikuwa na ajenda yao dhidi yangu. MwanaHalisi waliamua kunimaliza kisiasa. Hata hivyo kwangu mimi hayo yamepita, ni historia.
Mazungumzo yetu yalikuwa yanahusu nini? Yalikuwa yanahusu nchi. Watu wa Usalama wanasema tunawashambulia sana kwenye mikutano yao na wao sio wanasiasa kwa hiyo mara kwa mara wanajaribu kutusihi tusiwazungumze. Tusiwataje taje. Mara zote nawaambia tutawataja pale ambapo wao wanahusika na kwamba hawapaswi kuhusika na CCM maana wao wanapaswa kulinda dola na sio kulinda CCM.
Wakati nipo Mwanza mapema mwaka 2011 palitokea mauaji ya raia yaliyofanywa na polisi kule Arusha, viongozi wetu wakakamatwa. Mmoja wa waliokamatwa ni Mzee Ndesamburo, mzee wa zaidi ya miaka 75 na wakawa wanamweka katika mazingira mabaya, niliwapigia watu Usalama kuwaambia kuwa hayo ni makosa. Wamwache mzee yule na wanataka kumshikilia wamshikilie nyumbani kwake, sheria zinaruhusu.
Wakati mwingine watu wa usalama wana shida zao pia maana wao ni Watanzania kama sisi.
Kwa mfano, Mwaka 2009 tulikuwa tunapitisha sheria ya Baraza la Usalama wa Taifa. Wakaja kuniomba kuwa sheria ile mbaya na inajaza watu wengi kwenye chombo hicho. Tuka mobilise wabunge kuikataa. Haikukatiza kwenye floor. Mwaka 2008 waliomba sheria yao iboreshwe ili kuondoa kipengele kinachowazuia wao kukamata. Maana sheria ya sasa inasema wao kazi yao ni kushauri tu. Nakumbuka nilifanya kazi hiyo na MwanaKijiji, alinisaidia sana kutafiti na kuandika kwa uzoefu wake wa Marekani kipengele kipya. Hatukufanikiwa na hivi sasa TISS hawana meno!

K:
Zitto na wabunge wanaokaa kwenye bodi za mashirika:
Je, unaonaje kama utajiandaa
kupeleka ‘Hoja binafsi’ Bungeni ili Bunge liazimie kwamba ni marufuku kwa
Wabunge kuwa Wajumbe wa Bodi za Wakurugenzi wa Mashirika ya Umma? Sina hakika
kama Wabunge watakubali kwa kuwa ni wanufaika lakini kama utapeleka hoja yako
kimahiri sina shaka litakubaliwa.
Ushauri mzuri sana. Lakini suala hili sio tu hoja
binafsi, suala hili nimewahi kuliandika muswada binafsi zaidi ya mara 4
Bungeni. Mtu yeyote anayefuatilia Bunge atakuwa anajua kuwa kwenye taarifa zote
za Kamati ya Bunge ya POAC tumekuwa tukipeleka maazimio haya kwamba wabunge
wasiwe wajumbe wa bodi za mashirika ya Umma. Miswada yangu yote ilipigwa chini
isipokuwa nilifanikiwa kwenye muswada wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ambapo hoja
yangu ilipitishwa na Bunge (sijui hawakujua maana sikupata upinzani kabisa).
Lakini nashukuru kuwa baadhi ya Mawaziri wametekeleza agizo la kamati yetu kuwa Wabunge wasiwe kwenye Bodi za Mashirika ya Umma. Waziri Muhongo Kaunda upya bodi ya TPDC, hakuna Mbunge. Waziri Mwakyembe Bodi ya TPA hakuna Mbunge. Waziri Kagasheki kuna Bodi Kaunda hakuna Mbunge.
Toka POAC ilipoanza juhudi hizi mwaka 2009, kuna mafanikio kidogo lakini tunahitaji kuhakikisha kuwa hili haliruhusiwi kabisa. Wabunge wabaki wabunge tu. Kwa hiyo nashukuru kwa ushauri ingawa tayari ushauri huu nimeshautekeleza sio kwa hoja binafsi, bali kwa muswada binafsi unaotunga sharia. Hivi sasa tuna muswada wa Sheria ya Ofisi ya Msajili wa Hazina na tumeweka kifungu hicho. Tutafanikiwa kuweka misingi ya utawala bora.
Ni kinyume na misingi yote ya utawala bora wabunge kuwa wajumbe wa Bodi za Mashirika ya Umma.

L:
Zitto na posho la wabunge:
Najua msimamo wa Chama chako
juu ya posho ni kuzipinga, je Chama chako kinatekelezaje msimamo huo kwa
vitendo?
Naomba swali hili aulizwe Msemaji wa Chama
Bungeni ambaye ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni. Mimi ninajisemea binafsi. Ninatekeleza
msimamo huu kivitendo. Sipokei posho za vikao Bungeni na mahala popote ambapo
ninahudhuria vikao kama sehemu ya kazi yangu. ( huu ni mfano wa namna
ninavyokataa posho #1 Say NO to Posho! « Zitto na Demokrasia)
Posho za vikao ni wizi wa fedha za umma. Posho za vikao ni moja ya dalili za mfumo unaoitwa ‘rent seeking ’ au Pato-nyemelea. Huu ni mfumo wa kujipatia kipato bila kufanyia kazi. Wabunge wamechaguliwa kwa kazi maalumu na tunalipwa mshahara na marurupu mengine kwa kazi hii. Kulipwa posho ya kukaa kitako ni kujipatia kipato bila kufanyia kazi. Wabunge wanakuwa kama genge la majambazi yanayovamia benki na kuiba! Kwa kuwa mfumo unatoa nguvu kwa wabunge, basi hawatumii silaha, bali wanatumia mfumo kujilimbikizia mali. Sitting allowances ni uporaji.

Je, katika suala hili ulipata
ushirikiano wa kutosha toka kwa wapinzani wenzako bungeni?
Ndio
maana tulikaa kikao na kuamua kuandika barua kwa Spika ili atupe fomu nyingine
za mahudhurio na nyingine za posho. Hajafanya hivyo na mimi siandiki
mahudhurio. Mimi kama Waziri kivuli wa Fedha nilikuwa nazungumzia na kutekeleza
msimamo wa kukataa posho kama sehemu ya kazi yangu. Ndio mandate yangu. I
walked the talk. Wengine watajisemea wenyewe maana mimi sio msemaji wao na wala
sio msemaji wa Wabunge wa upinzani.
Je, ulipata ushirikiano wa
kiwango gani toka kwa Wabunge wa CCM?
Mbunge pekee wa CCM aliyekuwa na msimamo kama
wangu ni ndugu Januari Makamba. Alishambuliwa sana kwenye chama chake lakini
alisimama kidete. Nafurahi kuona wabunge vijana kama hawa ambao wanaleta aina
mpya ya siasa. Ninamtakia kila la kheri. Ndugu Filikunjombe alinipa moyo sana
kuhusu suala hili lakini sikumbuki kama naye aliacha kuchukua posho. But he was
on my side all the time. January najua alikataa kuchukua posho. Wengine sijui.
Je, hadi sasa hupokei posho za
vikao?
Sipokei posho ya kikao (sitting allowances) na
sitapokea posho hiyo katika kipindi chote ambacho mimi ni Mbunge. Nikiwa Rais
moja wa uamuzi wangu wa kwanza utakuwa ni kufuta posho za aina hii kwenye
Serikali nzima. Nisipokuwa Rais nitamshawishi Rais atakayekuja afute posho hizi
na kuelekeza fedha tutakazookoa kwenye kuondoa umasikini vijijini.
M:
Umeme na Gesi
Una maoni gani kuhusiana na
hali ya umeme nchini kwa wakati huu? Itaichukua Tanzania miaka mingapi kuwa na
uhakika wa upatikanaji wa nishati ya umeme?
Nimekuwa
nikitoa maoni yangu kuhusu suala la nishati ya Umeme nchini toka nimekuwa
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya POAC. Suala hili wakati mmoja lilitaka
kunimaliza kabisa kisiasa kwani msimamo niliochukua niliamua ni msimamo mzuri
lakini haukupendwa na wengi ( Sakata
la Ununuzi wa Mitambo ya Dowans: Barua ya Zitto kwa Watanzania ).
Bila nishati ya umeme ya uhakika hatuwezi kabisa kukuza uchumi na kuondoa umasikini nchini. Serikali ikiamua baada ya miaka 3 hatutakuwa na tatizo la umeme. Serikali itulize akili kuhakikisha miradi ya Kiwira, mchuchuma na Liganga na mradi wa bomba la gesi unakamilika. Lakini pia Serikali isiwe kigingi cha players wengine kwenye sekta ya umeme na hasa uzalishaji. Serikali ingejikita sana kwenye kusamabza miundombinu na kuruhusu watu binafsi kuzalisha umeme mwingi. Hata hivyo suala la mikataba ya kununua umeme (PPAs) inabidi kuangaliwa vizuri maana mingi inanyonya nchi. Huko tuendako mikataba yote ya aina hii iwekwe wazi kama njia ya kuepuka ufisadi na kuimarisha uwajibikaji. Tanzania inaweza kuwa net energy exporter in the region. Uamuzi ni wetu.

Pia uliposema mikataba iwekwe
wazi, ulikuwa na maana gani? Ulimaanisha ikiwekwa wazi hata sisi wananchi wa
kawaida tutaweza kuiona ama ulimaanisha iwe wazi kwa wabunge peke yake?
Mikataba
iwe wazi kwa wananchi kuweza kuona wakati wowote. Pia itengenezwe nakala za
lugha rahisi ili wananchi wa kutoka kwenye maeneo yenye gesi wajue ni nini haki
zao na nini wajibu wao. Uwazi wa Mikataba ni silaha kubwa sana ya kupambana na
uporaji wa mali asili ya nchi. Uporaji mbaya zaidi ni uporaji dhidi ya kizazi
kijacho. Sitaki watoto wetu waje kwenye makaburi yetu kutulaani bali kutuombea
dua. USIRI unalea ufisadi.
Kama ni wabunge peke yake ndio waone mikataba hii, hilo litaleta utofauti gani kwenye bunge ambalo wabunge wake wanapiga kura za maamuzi kutokana na chama na si maslahi ya taifa?
Kama ni wabunge peke yake ndio waone mikataba hii, hilo litaleta utofauti gani kwenye bunge ambalo wabunge wake wanapiga kura za maamuzi kutokana na chama na si maslahi ya taifa?
Una maoni gani juu ya sera ya
Nishati ya Gesi kutafsiriwa kwa Kiswahili?
Tulitoa kauli kupitia Waziri wetu kivuli wa
Nishati kuwa Sera ya Gesi iwekwe kwa lugha ya Kiswahili. Imewekwa. Natoa wito
kwa watanzania wajadili na kutoa maoni namna ya kuhakikisha kuwa gesi inakuwa
kwa maendeleo ya nchi na sio kwa ajili ya watu wachache.
Kwa ujumla nimeandika sana kuhusu suala la mafuta na gesi. Makala hii ( https://zittokabwe.wordpress.com/tag...-gas-sector-2/) inaweza kusaidia ufahamu wa sekta hii na mwono wangu kama Mtanzania. Pia unaweza kwenda kwenye blog yangu utakuta blogposts nyingi sana kuhusu suala hili.
Napenda kuona Tanzania inakuwa nchi ya kupigwa mfano duniani kwa namna ilivyotumia utajiri wake wa gesi na Mafuta. Sitaki turudie makosa tuliyoyafanya kwenye sekta ya Madini. Nitaendelea kufuatilia kwa karibu sana sekta ndogo ya gesi na nitakuwa muwazi sana ili kuzuia 'a nigeria' in Tanzania.

N:
Zitto katika Uongozi/Ubunge na Urais 2015
Naomba kujua ni kwanini hasa
umekuwa na uamuzi wa kuachana kabisa na Ubunge na kutogombea tena; na kama hayo
ni maamuzi yako na hujaeshinikizwa na kitu ama mtu yeyote. Je utaendeshaje
maisha yako ya kisiasa nje ya Bunge na nje ya taasisi ya Urais?
Wakati
nagombea Ubunge mwaka 2005 niliwaambia wapigakura wangu kuwa nitakuwa Mbunge
wao kwa vipindi viwili tu. Niliwaambia nina ndoto za kuja kuwa Rais wa nchi
yetu baadaye. Hivyo haya ni makubaliano yangu na wapigakura wangu. Nia yangu ni
kupisha wengine nao wakimbize kijiti cha maendeleo ya Jimbo letu na Mkoa wetu.
Nimesema mara kwa mara kwamba ukiachana na siasa kazi ninayoipenda zaidi ni
ualimu. Nitakapomaliza Ubunge na Urais nitakwenda kufundisha. Ninajiandaa
vilivyo kwa suala hilo. Nitapenda kufanya tafiti, kusoma, kuandika na
kufundisha. Hivi sasa tunaandaa mpango wa kuanzisha Chuo Kikuu cha Ziwa
Tanganyika (Lake Tnaganyika University) mkoani Kigoma. Nitafurahi kama nitakuwa
mmoja wa wahadhiri wa mwanzo wa chuo hiki kufundisha Watanzania Uchumi wa
Rasilimali.
Sina wasiwasi pia wa kuendesha maisha maana mimi ni mwanachama wa NSSF, ninajichangia kwa hiari toka nilipoacha kazi katika Shirika la FES mwaka 2004. Ikifika mwaka 2015 nitakuwa nimetimiza ‘points’ za kulipwa pensheni. Nashukuru kwamba nilikwepa ushawishi wa kujitoa kwenye mafao. Naamini nitaendesha maisha yangu kwa kazi za kufundisha, kuuza vitabu, consultancies na pensheni niliyojiwekea akiba.

CHADEMA kina utaratibu gani wa
kutangaza nafasi za wagombea katika ngazi mbali mbali hasa ya urais?
Chama
chetu hakina utaratibu wowote hivi sasa wa kutangaza nia za watu kutaka
kugombea nafasi yeyote. Juzi tumekutana Morogoro na kukubaliana kuwa
tutatengeneza utaratibu wa watu kutangaza nia zao wanapootaka kugombea nafasi
yeyote ya uongozi. Nadhani huu ni uamuzi mzuri wa chama maana kuna watu wana
wasiwasi usio na msingi kabisa kuwa kuwa na wagombea wengi kwenye chama ni
kuvuruga chama. Lakini watu hao hao wanashangilia kweli wakiona demokrasia
inavyotekelezwa kwenye nchi nyingine kama Marekani. Watanzania wanapenda kuona
demokrasia inatekelezwa lakini wanaogopa kuitekeleza wao. Uamuzi wa Morogoro
kuhusu mwongozo kwa wagombea utatusaidia sana kuondoa mashaka kama haya.
Katika moja ya ‘school of
thought’, inasemekana umetangaza haraka nia ya kugombea Urais kwa misingi ya
kuwa Dr. Slaa hana tena mpango huo na kwamba nje ya Slaa huoni zaidi yako
ambaye anaweza wakilisha vema. Unalizungumziaje hili mkuu?
Slaa
hakuwahi kutangaza nia ya kugombea Urais wakati wowote ule wa maisha yake.
Mwaka 2010 Tulimwomba kama chama. Chama kinaweza kumwomba tena na tukifikia
mwafaka ndio atakuwa huyo na sote lazima tumwunge mkono. Mimi nimetangaza kwa
kuwa ninautaka Urais na hivyo nakiomba chama kiniteue. Pia chama kina viongozi
wengine wazuri tu. Tundu Lissu na Mnyika wamesema hawautaki Urais. Ndugu Mbowe
yeye hajasema kama anautaka au la. Kumbuka hata mwaka 2005 Mbowe
tulimlazimisha, yeye alitaka aendelee kuwa Mbunge wa Hai. Sisi tukamwambia kuwa
lazima abebe chama. Nakumbuka mimi binafsi niligombana naye maana aliposema
yeye atagombea Hai, nikamwuliza kwa chama gani? Maana kama hutaki kukibeba
chama kwenye Urais tutachukua kadi yetu. Ndio! Nilimwambia hivyo kwenye
secretariat ya chama. Akakasirika kweli, lakini baadaye alinielewa na mafanikio
tuliyoyapata ni makubwa sana baada yeye kugombea. Kwa hiyo hiyo School of
Thought ni hisia tu za watu. CHADEMA ina watu wengi sana wenye uwezo wa kuwa
maRais. Kitila Mkumbo mnamwonaje? Au mpaka watu wawe Bungeni. Huyu ni hazina ya
chama na nchi. Chama kinaweza kusema, Zitto hapana, mwunge mkono Kitila.
Nitafanya hivyo. The Party deploys for or against your wishes and every
member must oblige a JUST deployment. I will.
Ikitokea kuwa hujateuliwa na
chama chako (CHADEMA) kugombea Urais 2015 kwa tiketi ya chama hicho, una nia ya
kutafuta chama kingine kitakachokuruhusu kugombea nafasi hii ya Urais?
Nisipoteuliwa na chama kugombea Urais nitamfanyia
kampeni mgombea atakayeteuliwa na chama. Siamini katika kuhama vyama ili
kutimiza malengo ya kisiasa na ndio maana mimi sijawahi kuwa chama kingine
chochote zaidi ya CHADEMA maisha yangu yote. Mwanasiasa anayehama vyama ili
kupata uteuzi anafuata vyeo na sio muumini wa sera ya chama husika.Vile vile
Urais kwangu mimi sio an end in itself, it is a means ya kuleta mabadiliko ya
hali ya maisha katika nchi yetu. Kama ilivyokuwa kwa Ubunge, ambapo nimehudumia
wananchi na kuleta mabadiliko makubwa sana ndani ya muda mfupi na sasa nataka
kuachia wengine, Urais nao ni hivyo hivyo, kutaka kufanya transformation ya
nchi yetu, radical transformation katika uchumi, siasa na jamii. Nataka
kuionyesha dunia kuwa tunaweza kuondokana na umasikini in our life time. Sasa
kama chama kina mtu mwingine mwenye mwona kama huu, mimi nitamuunga mkono na
kumsaidia kuifanya kazi hii.
Kabla ya uchaguzi wa 2010 ulishawahi tangaza kutogombea tena ubunge 2010; ni kitu gani kilifanya ubadilishe huo msimamo?
Mwaka
2009 niliamua kuwa ni bora niache ubunge ili nifanye shahada yangu ya uzamivu
na kasha nifanye machapisho. Unajua niliingia Ubunge nikiwa na umri wa miaka 29
tu. Kazi niliyofanya kwenye Bunge la Tisa ilikuwa inanizidi kimo kwa kweli.
Nilikuta Bunge limelala sana. Lilikuwa Bunge la status quo. Halikuwa Bunge
vibrant kabisa. Siku ya kwanza tu nimeingia Bungeni sikulipenda. Hamu
iliniisha. Lakini nikasema ngoja nibadili modus operandi ya Bunge. Nikaanza
kutoa hoja kali kali Bungeni na hatimaye nikasimamishwa Bunge. Nafurahi kwamba
Wabunge wengine walifuata kasi yangu. Mnakumbuka kuna wabunge walikuwa wanasema
‘hatuwezi kumwachia Zitto Kabwe peke yake kazi ya kuibua ufisadi’ nk. Sasa
baada ya kuona nimefanikiwa nikasema basi term moja inatosha. Badaye nikapata
ushawishi kuwa hapana, nenda Geita au Kahama au Kinondoni. Nikafanya utafiti
wangu nikaona mwenyewe kuwa niende Geita. Viongozi wa chama kutoka Geita
wakaenda kuwaona wenzao Kigoma wakakataliwa. Wazee wakanikumbusha kuwa,
makubaliano yetu yalikuwa mihula 2. Ikabidi nitimize ahadi hiyo ya mihula 2.
Haikuwa matakwa yangu. Mpaka sasa nime abandon PHD yangu maana sina muda na
siasa zangu mimi huwa naacha kila kitu kinacho weza kuni divert, hivyo nakosa
muda wa kusoma na kuandika.
Tokana na kauli yako hivi
karibuni kuhusu kwamba Uongozi wa nchi hautakiwi kuwa mikononi mwa watanzania
waliozaliwa kabla ya uhuru; Je kulikuwa na ulazima kutamka haya? Huoni kwamba
iwapo utafanikiwa kuwa rais wa nchi yetu, urais wako unaweza kuja kutuletea
generational conflicts (misuguano/migongano/mifarakano ya vizazi)?
Mimi ninaamini kabisa kuwa Rais ajaye wa Tanzania
ni lazima atokane na kizazi cha baada ya uhuru. Nchi inahitaji a fresh start.
Misuguano ndio huleta maendeleo. Hebu tazama nchi hii, Asilimia 70 ya
Watanzania wapo chini ya umri wa miaka 29! Asilimia 65 ya wapiga kura wapo kati
ya umri wa miaka 18 – 40. Hili ni Taifa la vijana. Nusu ya Watanzania wapo
chini ya umri wa miaka 17! Unaweza kusema hili ni Taifa la watoto. Hawa wazee
wetu walipokuwa wanachukua nchi walikuwa vijana. Mwalimu alikuwa Waziri Mkuu
akiwa na miaka 39, Mzee Kawawa alikuwa Waziri Mkuu akiwa na miaka 37. Waziri
Mkuu wakati huo ndio alikuwa Mkuu wa Serikali maana Mkuu wa nchi alikuwa Malkia
wa Uingereza. Angalia mafanikio ya Mwalimu Nyerere na Kawawa kati ya mwaka 1961
na 1971 halafu pima na baada ya hapo mpaka wanastaafu. Tusibwabwaje tu bila
evidence. Ndio maana leo Marekani Rais wao ni kijana. Uingereza Waziri Mkuu wao
kijana ingawa mataifa haya yana wazee wengi zaidi kuliko sisi. Ninaweza kutamba
kwamba mimi ni mmoja wa wanasiasa ambao ninaheshimu sana wazee. Uliza wazee
waliopo na waliokuwapo Bungeni ni mwanasiasa gani kijana anatumia muda mwingi
nao. Mwulize mzee Sarungi, bahati mbaya mzee Makwetta amefariki. Mwulize dokta
Salim, mwulize Mzee Warioba. Wao pia wananiambia, Zitto huu ni wakati wenu.
Sisi tulifanya yetu.
Kuna watu lazima watafsiri chochote atakachosema Zitto. Hata hili ninaloandika hapa mtasikia, watasema tu. Kuna watu wanaumwa ugonjwa wa zittophobiasis ni lazima waseme. Mtasikia tu wanasema hivi sasa. Sasa wanaotaka kutafsiri kauli yangu wana mambo yao, lakini ninaamini kabisa kuwa changamoto za sasa za Taifa zinahitaji Rais wa kizazi cha baada ya Uhuru. Wazee watatupa ushauri. This country has to move very fast. We need an ambitous young man, visionery and focused to transform this country. Tunaweza kuwa na Spika mzee ili adhibiti kasi kama inakwenda sana, lakini sio CEO wa nchi. How Old was Lumumba? How old was Kagame? How old is Kabila?
Let us be serious guys. Mnataka tutambae? Wazee wameishi maisha yao. Wameishi yetu na sasa tunataka kuwakopesha maisha ya watoto wetu?

O:
Zitto na "Ufisadi na Malimbikizi ya Mali" & "Pesa Uswisi"
Unaposema kuwa ni jitihada zako
mwenyewe za kupata hayo majina ya mafisadi wa Uswisi si inakuwa sawa na kuwa
una maslahi yako binafsi kama vile kutaka kuyauza hayo majina kwa wale ambao
wapo kwenye list?
Nadhani
hivi ndivyo ungefanya wewe maana wakati mwingine watu hudhani vyao kwa wengine.
Unachukuliaje mawazo/kauli ya
baadhi kuwa kuwasilisha kwako hoja hiyo ya fedha za Uswizi bungeni bila kutaja
majina ni moja ya njia ya kujisafisha katika uvumi/tetesi ya kuwepo katika list
hiyo ya wenye fedha Uswizi?
Kwangu
mimi suala hili ni pana na majina ni sehemu tu ya suala hili. Nimeshasema mara
kadhaa kwamba, nina akaunti mbili hapa nchini, CRDB na NMB. CRDB kwa ajili ya
mshahara wangu na NMB kwa ajili ya fedha za kujikimu ninazolipwa na Bunge. Sio
tu Uswisi, hapa Tanzania sina akaunti benki nyingine yeyote ukiachana na kuwa
signatory kwenye akaunti za chama au za kifamilia.
Sina biashara yeyote hapa nchini au nje ya nchi. Naishi kwa mshahara na siwezi kuupeleka mshahara Uswisi. Waliosema mimi nina fedha huko Uswisi walikuwa na lengo la kufifiza hoja yangu kwa malengo yao. Ni watu waliotumwa na usalama wa Taifa au na wenye fedha ili niogope. Watu wa aina hii ni wapuuzi, wapumbavu na hatari sana kwenye vita dhidi ya ufisadi. Tena watu hawa mnawajua na mnawachekea. Hawa watu ni vibaraka wa watu fulani. Tena nasikia wametengeneza na orodha yao ya wenye fedha nje. Hawa ndio wagonjwa wa zittophobiasis. Nasikia wengine walisema kuwa hii hoja akiachiwa Zitto itampa umaarufu. Wapuuzi wanawaza umaarufu tu badala ya kuwaza nchi yetu.
Suala la utoroshwaji wa fedha kwenda nje ni kubwa sana. Tanzania imepoteza dola bilioni 11 toka mwaka 1970 mpaka sasa (ukiongeza na riba kwenye fedha hizo). Halafu kuna wapuuzi fulani wanaleta uzezeta kwenye masuala ya msingi ya nchi. Wanajijua ninaowasema hapa. Waache ujinga. Kama humpendi Zitto basi penda afanyacho kwa maslahi ya nchi yetu.

Kuna ukweli wowote kuwa taarifa
ile ya USWISI kuiwekea masharti Tanzania, ilitoka ndani ya serikali ya USWISI au
ni mkakati wa mafisadi hawa kuzima jaribio la kurejesha pesa hizo?
Nimetoa
kauli jana kuhusu suala hili. Nimesema Watanzania tusiwe mazezeta. Kauli hizi
ndio ambazo hata Marekani waliambiwa. Hata Ujerumani waliambiwa. Sisi
kuzishabikia badala ya kufanya uchunguzi wetu kwa njia zetu ni dalili za kutaka
kuua hoja hii. Hoja hii haitakufa. Tutaisimamia mpaka mwisho.
Je, kuna nafasi ya nchi yetu
kufanikiwa kuyarejesha mabilioni hayo ambayo ni kodi ya wanachi?
Tunaweza
kurejesha. Kuna Azimio la Bunge na nitahakikisha Azimio la Bunge linatekelezwa.
Senegal wanafanikiwa sana. Kenya walifanikiwa kwa kutumia wachunguzi binafsi.
Kama Serikali ya CCM itashindwa kufuatilia suala hili, Serikali ya CHADEMA
itafanya hivyo. Hawana pa kujificha katika dunia ya sasa.
Ikumbukwe kuwa, tangu nchi hii
itumbukie ktk ufisadi mkubwa, chombo chetu TISS kipo kama hakipo, na kama kipo
basi ni kwa msaada wa mafisadi tu, Katika mtazamoo na tafsiri ya ripoti yako,
taasisi ya Usalama wa Taifa (TISS) Unaiweka katika mizani ipi au haihusiki
katika hili?
Idara
ya Usalama wa Taifa ni lazima isaidie nchi kwenye masuala kama haya, vinginevyo
hawapaswi kuwepo. Sheria ya TISS ya mwaka 1996 inawazuia kuchukua hatua fulani
fulani. Tutarekebisha sheria hiyo. CCM wasiporekebisha sisi CHADEMA tutapata
ridhaa ya wananchi kuiandika upya sheria ya Usalama wa Taifa. Tunataka usalama
wa Taifa na sio usalama wa viongozi au vyama vya siasa.
Kwanini umependekeza kuundwa
kwa tume, na kuendelea kumaliza pesa za watanzania wakati kimantiki ripoti yako
ilikuwa ni ya kuiwasilisha vyombo vya dola tu, na ikiwa hawajaridhika, TAKUKURU
kwa utaratibu wao wa ndani waendeshe uchunguzi na kuchukua hatua?
Uzuri
wa Kamati Teule ya Bunge ni kwamba kila kitu huwa wazi kwenye hansards za Bunge
na hivyo ni rahisi kufichua uchakachuaji. Pia ngoja niwamegee siasa za Bunge
kidogo. Bungeni unapokuwa na hoja unaingia na hitaji kubwa sana wakati unajua
fall back ni nini. Tulijua kwa hatua ya sasa hawatakubali kuundwa kwa kamati
teule, tulitaka hoja ipite ili kujenga msingi wa kupanua uchunguzi siku za
usoni. Tukafanikiwa. Tulitumia approach hiyo hiyo kwenye hoja ya ndugu Halima
Mdee. Ni mikakati tu. Sisi tumekuwa ni Bunge la kwanza katika eneo la SADC
kutoka na Azimio kuhusu 'illicit money flows'. Sasa tunapaswa kuhakikisha
Azimio linakuwa enforced na kisha a public inquiry....
Huku ukijua serikali haina nia
ya kuwataja walioficha fedha mabenki ya nje huku wewe ukiwa na majina;
unayashikilia hadi sasa ili nini na kwa faida ya nani?
Kwa
faida ya uchunguzi. Lazima Serikali ijenge uwezo wake wa kuchunguza na kuweka
mambo sawa baada ya uchunguzi. Sasa ikiwa mimi kama mbunge nitatoa jina la
walio torosha pesa kwa sasa, nani atatoa majina hapo kesho? Mbunge mpya wa
Kigoma kaskazini?
Yale majina ya baadhi ya
watanzania unaowatuhumu kumiliki fedha haramu/halali (nyingi) nje ya nchi
kwanini huyaweki bayana kwa umma? Wewe kama Mtanzania mzalendo na nchi yako
kwanini umeshindwa (na chama chako) kuwapeleka mahakamani na kuwafungulia
mashitaka?
Uchunguzi
bado unaendelea
Kulikuwa na tetesi kuwa nawe
umeficha fedha nje. Hii inaweza kulenga kukuchafua ili uwagwaye waliofanya
hivyo, je huoni kuwa hii ni nafasi adimu ya kuondoa shaka? Tuondoe wasiwasi
katika hili…
Sina fedha za kuficha nje. Nazitoa wapi? Sina
biashara naishi kwa mshahara wa ubunge, natoa wapi fedha za kuficha nje?
Kwanini ulipeleka hoja binafsi
ndani ya bunge na si kupitia uwakilishi wa upinzani? Je, umefanikiwa kwa kile
alichotaraji kutokana na hoja hii? Uliungwa mkono na chama?
Sijaelewa
swali lako. Mimi ndio Waziri kivuli wa Kambi ya Upinzani kuhusu Fedha. Upinzani
gani tena? Unadhani chama makini kama CHADEMA kinaweza kuacha mbunge wake
apeleke hoja bungeni bila kuungwa mkono na chama? Wale wabunge waliosimama
kuunga mkono niliposema 'naomba kutoa hoja' ni wabunge wa CHADEMA wale(isipokuwa
ndugu Kessy na Kangi Lugola ambao ni CCM).
Vipi, unauongeleaje ujenzi wa
bandari ya Bagamoyo?
Ni wazo zuri lakini lifuate mpango wa Ports
Masterplan. Sio suala jipya hili.
P:
Zitto katika Maswali Mchanganyiko
Nini uelewa wako kuhusu
familia? Umeoa? Maana Kuishi au kuwa na mke siyo jambo jepesi, linahitaji
uvumilivu na busara nyingi sana, kama vile ilivyo kuishi na mume. Kama hili
limekushinda, vipi utaweza kuwaongoza watanzania wote wake kwa waume?
Ninaamini
katika familia imara na ni mwumini wa familia ya kiafrika ambapo familia sio tu
ni mke, mume na watoto bali pia ndugu na jamaa mbalimbali. Ndio maana ninaishi
na ndugu zangu, nimelea wadogo zangu na wazazi wangu na hivi sasa ni nguzo
katika ukoo wetu mkubwa sana ambao kuuweka pamoja kunahitaji uvumilivu na
busara nyingi sana kuliko hata busara inayohitajika kwa mke na watoto. Mimi
sijaoa. Muda ukifika nitaoa. Sitaoa kwa sababu ya kuonekana kiongozi ameoa.
Nitaoa pindi nitakaporidhika na huyo mwenzangu ambaye nitafunga naye ndoa.
Historia inatuonyesha viongozi wengi sana ambao wameoa na wameshindwa kuongoza
nchi zao. Vilevile tuna viongozi wengi sana ambao hawana wake au waume na
waliongoza nchi zao vizuri sana.
Indira Gandhi hakuwa ameolewa kipindi chote akiwa Waziri Mkuu wa India. Baba yake Indira, Nehru naye alikaa miaka zaidi ya 30 bila mke. Rais Khama wa Botswana hana Mke wala mtoto, hajapata kuoa lakini anaendesha nchi yake kwa mafanikio makubwa sana kuliko King Mswati mwenye wake zaidi ya 12. Rais Nkrumah alioa mwanamke ambaye hakuwa anamjua akiwa tayari ni Waziri Mkuu wa Ghana, tena aliletewa mke na Rais Nasser wa Misri. Hakuna mahusiano yeyote ya kisayansi kati ya kuoa na uongozi mzuri ingawa kuoa ni muhimu sana. Sidhani kama kuoa itakuwa kikwazo katika uongozi wangu kama itafikia uchaguzi sijaoa maana tumeona viongozi kadhaa wakiamua kuoa baada ya chaguzi. Hata hivyo nitafurahi zaidi kuoa kabla sijawa Rais, lakini ikibidi nitaoa nikishakuwa Rais. Sitalazimisha ndoa kwa ajili ya Urais. Nitaoa nitakapopenda kuoa.

Mkuu Zitto is there any chance
unajua mshahara wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mshahara wa makamu
wa rais wa JMT, na ule wa rais wa Zanzibar? Ni mahala gani pa kwenda kufuatilia
hizo data kwa yeyote yule anayetaka kufahamu hayo? Pia katika hili unadhani ni
kwanini hiyo mishahara inawekwa siri sana kwa wananchi hali kimantiki wananchi
ndio waajiri wao?
Sijui
mshahara wa Rais na naamini ni katika vitu ambavyo walipa kodi wanatakiwa
kujua. Mshahara wa Rais hautakiwi kuwa siri kwa mtanzania yeyote. Inapaswa kuwa
wazi kabisa na kila Raia ajue. TRA watakuwa wanajua kama sio tax exempt.
Nadhani tukifatilia kupitia Utumishi tunaweza kupata hizo data. Hebu ngoja
nipeleke swali Bungeni kuhusu jambo hili ili lijibiwe Mkutano ujao wa Bunge.
Haya ni mambo ambayo tuna overlook sana.
Mwaka 2008 wakati tunapitisha sheria ya Utawala wa Bunge (National Assembly administration act) niliwasilisha ammendment kuwa mishahara ya wabunge na mawaziri iwe wazi na iwekwe online watu waweze ku access. Nikajibiwa ni siri ya mtu. Rais ni mtu ndio, lakini sio mtu kama mtu mwingine. Ni mtu mwenye maamuzi kuhusu mwelekeo wa Taifa. Ni vizuri kujua tunamlipaje. Ngoja na mimi niwaulize, Nani anajua mshahara wa Mbunge wa Jimbo lake hapa?

Mkuu unadhani unakubaliana na
mfumo wa Uongozi wa serikali uliopo sasa? Kama HAPANA unadhani ni mfumo upi
ambao ni mzuri na unafaa kwa kupata viongozi wa vyama vyetu kwa ngazi za juu
kama M/Kiti, Makamu M/Kiti na Katibu Mkuu – Ule wa kuteua na kupigiwa kura za
wajumbe au kugombea na kupigiwa kura na wajumbe na kwanini?
Sina maoni
Ni ukweli kuwa wewe ni mshauri
wa uchumi wa Ujerumani. Kama ni kweli, je ni kitu gani kilichokutambulisha hadi
kufikia kupewa hiyo nafasi?
Nilikuwa
kwenye jopo la Rais Kohler kuhusu Afrika. Nilimaliza kazi hiyo mwaka 2009.
Niliteuliwa tu na Rais Kohler wa Ujerumani
Umewahi kuanika utajiri wako
(vitu unavyomiliki); unaweza walau kutufafanulia unamiliki magari mangapi,
nyumba ngapi n.k?
Nimewahi
kusema ninamiliki nini ili kufuta uzushi unaoenezwa kuwa mimi nina ukwasi wa
kutisha. Nina gari 2, moja Freelander na nyingine Toyota vista. Ninajenga
nyumba Kigoma, kijijini Mwandiga. Nina shamba lenye mikorosho 400 Mtwara, Nina
shamba la ekari 3 eneo la Mbutu, Kigamboni. Ninadaiwa na CRDB milioni 120
nilizokopa kwa ajili ya kununua vitu hivyo. Nina mkopo wa Bunge wa kununua gari
wa tshs 90 milioni ambao tunalipa nusu yake! Nina exemption ya kodi ya kuingiza
gari lakini nimekataa kuitumia kwa sababu mimi kama Waziri kivuli wa Fedha
ninapinga tax exemptions na hivyo nimeamua ku walk the talk. Sijaitumia na sitaitumia
exemption hiyo.
Nimeamua kuwa ifikapo Mwezi January, mara baada ya kujaza fomu zangu za Maadili na kuziwasilisha nakala ya fomu hiyo ya Mali na Madeni nitaiweka online kwenye blog yangu ili kila mtu aone nimetangaza nina miliki nini na yeyote mwenye mashaka aweze kuniumbua kwa kusema mbona hili umeacha, mbona lile umeacha. Njia pekee ya kumaliza uzushi na majungu ni uwazi. Shaurini wabunge wenu wafanye hivyo pia ili kupambana na ufisadi.

Unazionaje shughuli za
kisayansi za watanzania? Je, kuna sera yeyote Tanzania inayompa kijana wa
kitanzania nafasi ya kuwa mbunifu?
Kuna sera na sheria za kusaidia ubunifu wa
kisayansi. Tatizo ni kwamba Tanzania hatuheshimu sana R&D issues na matokeo
yake tumekuwa watumiaji wa ugunduzi wa watu wengine. Kwenye eneo la ICT nimeona
vijana wameanzisha The Kinu, tutawasaidia. Hii platform hapa tunayotumia JF
imetengenezwa na Mtanzania Maxence, lazima tumsaidie ili iweze kudominate eneo
lote la maziwa makuu.
No comments:
Post a Comment