Taarifa kwa Vyombo vya Habari
SHIRIKISHO
la Mpira wa Miguu Tanzania limeteua wadau 10 kwa ajili ya kusaidia timu
ya taifa ya vijana walio na umri chini ya miaka 17, Serengeti Boys
itakayopambana na Congo (Brazaville) katika mechi ya raundi ya tatu ya
michuano ya awali ya Mataifa ya Afrika.
Uteuzi
huo umefanywa na Rais wa TFF, Leodegar Tenga baada ya Kamati ya Vijana
ya TFF kufanya kikao chake kujadili kwa umakini ushiriki wa timu hiyo na
kupeleka mapendekezo yake kwa rais huyo wa shirikisho.
Kutokana
na umuhimu wa mechi hiyo itakayoamua timu itakayofuzu kucheza fainali
za Mataifa ya Afrika, TFF imeona umuhimu wa kuwa na kamati ambayo
itakuwa na majukumu mawili makubwa ambayo ni:
1. Kuhamasisha vijana waone umuhimu na kuwa na ari ya kushinda mechi hiyo
2. Kuhamasisha umma uone umuhimu wa mechi hiyo na hivyo kuisaidia iweze kufuzu.
Walioteuliwa kuunda kamati hiyo ni:
1. Ridhiwani Kikwete Mwenyekiti
2. Ahmed Seif (Magari) Mjumbe
3. Nassoro Bin Slum Mjumbe
4. Henry Tandau Katibu
5. Ahmed Mgoyi Mjumbe
6. Aboubakar Bakhresa Mjumbe
7. Angetile Osiah Mjumbe
8. Kassim Dewji Mjumbe
9. Abdallah Bin Kleb Mjumbe
10. Salim Said Mjumbe
Baada
ya kuvuka raundi mbili za kwanza bila ya kucheza mechi kutokana na
wapinzani wake kujitoa, timu ya Serengeti Boys inahitaji kufanya kila
iwezalo kuweza kuiondoa Congo kwenye mashindano hayo na kuweka rekodi ya
kufuzu kucheza fainali hizo za Afrika ambazo pia zitatoa wawakilishi wa
Afrika kwenye mashindano ya Kombe la Dunia. Mechi za kwanza za raundi
ya tatu zitachezwa kati ya Novemba 16 na 18, 2012 na mechi za marudiano
zitachezwa kuanzia Novemba 30, 2012 hadi Desemba 2, 2012
*Kuhusu
suala la Azam FC kuwasimamisha wachezaji watatu kwa tuhuma za kuhusika
kuhujumu timu, tayari TFF imepokea barua hiyo ya Novemba 8, 2012 na
inalishughulikia na kulifuatilia kwa makini.
*TFF
inapenda kukipongeza Chama cha Mpira wa Miguu cha Mkoa wa Mwanza kwa
kufanya uchaguzi wake kwa amani na kufanikiwa kupata viongozi wapya
watakaokuwa chini ya uenyekiti wa Jackson Songora. Rais wa TFF
amewapongeza viongozi waliorekjea madarakani na viongozi wapya akieleza
magtumaini yake kuwa kamati mpya ya Utendaji ya MRFA itaelekeza nguvu
zake katika kuendeleza mikakati iliyokuwepo ya kuinua kiwango cha mpira
wa miguu na kubuni mikakati mingine kwenye mkoa huo na Tanzania kwa
ujumla ikishirikiana na TFF.
*Ligi Kuu ya Vodacom inatazamiwa kuendelea kesho kwenye viwanja tofauti
1. Simba v Toto Africans Uwanja wa Taifa
2. T. Prisons v JKT Ruvu Sokoine
3. Kagera Sugar v Polisi Moro Kaitaba
4. African Lyon v Mtibwa Sugar Azam Complex
5. Oljoro JKT v Ruvu Shooting Sheikh Amri Abeid
6. Mgambo JKT v Azam FC Mkwakwani
Jumapili
1. Coastal Union v Young Africans Mkwakwani
No comments:
Post a Comment