Maalum kwa habari mbalimbali za kisiasa, kiuchumi, kijamii, michezo na burudani pamoja na matukio.
Wednesday, April 4, 2012
Askari wa kikosi cha Zimamoto jijini Dar es Salaam wakiwa katika mazoezi yao katika kukabiliana na moto. Mazoezi hayo yanafanyika katika Kituo Kikuu chao kilichopo Fire.
Wabunge wa Kamati ya Kamati ya Hesabu ya Mashirika ya Umma (POAC) wakimsikiliza mtaalam wa mionzi kutoka TCRA Dk Ally akiwaonyesha kifaa kinachotumika katika kuchunguza mionzi kwenye minara ya simu wakati kamati hiyo ilipotembelea ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano nchini.
Monday, April 2, 2012
Mbunge wa Ilemela mkoani Mwanza, Highness Kiwia akipelekwa kupigwa picha ya X ray katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya uchunguzi zaidi kutokana na kupigwa na watu wasijulikana mara baada ya mkutano wa kampeni za udiwani jimboni humo
Thursday, March 29, 2012
Yanga yaipania Coastal Union
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga imeapa 'kufa na kupona' mjini Tanga watakapoumana na Coastal Union katika mfululizo wa ligi hiyo.
Yanga na Coastal zinatarajia kumenyana Jumamosi kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga ambapo kila timu inahitaji ushindi ili kujiweka pazuri katika ligi hiyo inayoelekea ukingoni.
Yanga na Coastal zinatarajia kumenyana Jumamosi kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga ambapo kila timu inahitaji ushindi ili kujiweka pazuri katika ligi hiyo inayoelekea ukingoni.
Subscribe to:
Posts (Atom)