·
Kulipia kodi ya mapato na majengo
·
Airtel na TRA kuwezesha ukusanyaji na ongezeko la mapato
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayotoa huduma za
mawasiliano yenye gharama nafuu zaidi na mtandao wenye wigo mpana leo imezindua
mwendelezo wa huduma za Airtel kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) kwa kuwawezesha wateja wake nchi nzima kulipia Kodi kupitia huduma ya
Airtel Money. Hii imekuja wakati huduma za pesa kutumia simu zimekuwa
zikibadilisha huduma za kibiashara na kuongeza ufanisi.
Kwa kupitia huduma ya Airtel money na ushirika na Mamlaka ya
Mapato Tanzania Airtel wateja wa makampuni hayo wataweza kulipia kodi ya mapato
na majengo kupitia Airtel Money.
Akiongea wakati wa uzinduzi uliofanyika makao makuu ya
kampuni ya Airtel, Mkurugenzi wa Biashara za Mashirika bi Irene Madeje Mlola
alisema” Airtel imekuwa mstari wa mbele katika kuleta ufanisi na mapinduzi
katika sekta ya mawasiliano nchini. Leo tuna furaha kushirikiana na Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) kwa kuwezesha wateja wake kulipa kodi kwa kupitia huduma
ya Airtel Money. Airtel money ni huduma iliyotengezwa kukithi mahitaji ya
wateja wetu na hii ni hatua nyingine muhimu kwa Airtel kutumia miundo mbinu
tuliyonayo na TRA katika kuhakikisha wanaboresha huduma zao. Sasa walipaji wa
kodi wadogo na wakubwa wanalipia kodi zao kwa urahisi wakiwa katika biashara
zao na nyumbani”
“Mpaka
sasa takribani nusu ya wateja wa Airtel wamejiunga na kutumia huduma ya Airtel
money, huduma iliyo rahisi, iliyojitosheleza, salama na nyenye kutoa nafasi
kufanya miamala mbalimbali ikiwemo malipo ya bidhaa mbalimbali. Kwa kupitia
huduma ya Airtel money inayotoa huduma nyingi zaidi ya kutuma pesa tumeona
maisha ya watanzania wengi yakibadilika kila siku na biashara zao kuwa na
ufanisi zaidi aliongeza Madeje.”
Kwa
upande wake Kamishina Msaidizi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania bw
Rished Bade alisema” Tunayofuraha kuzindua huduma yenye kutumia mfumo wa
teknolojia ya malipo ya uhakika na salama kwa wateja wetu nchi nzima.
Uzinduzi wa leo ni udihirisho wa juhudi za Mamlaka katika
kuongeza uboreshaji katika huduma za malipo ya kodi na ukusanyaji wa
mapato.Tunategemea kwa kupitia huduma ya Airtel Money kutawezesha ulipaji wa
kodi kwa wakati na kuwahamasisha watanzania wengi zaidi kulipia kodi zao za
mapato na majengo. TUnategemea kuona ongezeko kubwa la wafanya biashara wadogo
na wakati ambao leo hii wanalipia malipo ya kodi kwa kupitia maofisi na vituo
mbalimbali vya kodi nchi nzima.
Akiongelea kuhusu njia ya kulipia kodi hizo kwa njia ya simu
Meneja Uendeshaji Airtel Money Asupya Naligingwa alieleza”Kulipia kodi ya
majengo au mapato mteja wa Airtel atatakiwa kupiga namba *150*60#
kisha
- Atachagua
Lugha
- Atachagu
malipo ya bili
- Lipa Bili
- Atachagu
“JIna la fumbo” MAJENGO”
- Ingiza
kiasi cha fedha unachotaka kulipia
- Ingiza
neno la siri
- Ingiza namba ya akaunti ya Mamlaka ya Mapato (TRA) kisha
bonyeza OK na utapokea meseji(SMS)itakayothibitisha malipo yako ”
Huduma
ya Airtel Money service inayopatikana kwa kupiga *150*60# inawawezesha
wateja kulipia huduma mbalimbali zikiwepo kama vile za kulipia bili za maji na
umeme,bidhaa na huduma mbalimbali kama vile bima,kununua muda wa
maongezi,miamala ya huduma za kibenkiikiwemo kuweka na kupokea kutoa na vile
vile kulipia huduma nyingine nyingi.
Airtel
Money ni huduma inayopatikana masaa 24, siku 7 za wiki kutoka katika simu na ni
salama ya uhakika na rahisi kutumia. Kinachohitajika ni kitambulisho na usajili
wa simu yako ili kuweza kupata huduma hii katika maduka na mawakala wote
waliopo nchi nzima.
No comments:
Post a Comment