Mbunge wa Tanzania
ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano wa Chama cha Mabunge Duniani Mhe. Hamad Rashid
Mohamed ameteuliwa na kamati tendaji ya chama cha Mabunge duniani (IPU) kuwa
mjumbe wa kamati ndogo ya ukaguzi wa ndani kwa mahesabu ya mwaka 2013 ya chama
hicho.
Uteuzi huo ulifuatia pendekezo la umoja wa Mabunge ya
Afrika lililowasilishwa na katibu mkuu wake Koffi N’Zi tarehe 22 Oktoba, 2012
kufuatia kikao cha wajumbe wa umoja wa Mabunge ya Afrika kumchagua Mhe. Hamad
kuwakilisha Afrika kuwania pendekezo hilo
mbele ya kamati tendaji ya chama hicho.
Mhe. Hamad Rashid Mohamed, hii ni mara ya pili kuiwakilisha
Tanzania
na Afrika katika kamati mbalimbali za IPU ambapo mwaka jana katika Mkutano
uliofanyika Mjini, Benn, Uswis, alichaguliwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Fedha na
Uchumi ya IPU cheo ambacho anakitumikia hadi hivi sasa.
Katika kamati hiyo ya ukaguzi wa ndani, Mhe. Hamad Rashid
atafanya kazi pamoja na mjumbe mwingine aliyeteuliwa Mhe. Duarte Pacheko kutoka
Ureno, ambapo wanatarajia kutoa taarifa ya kazi yao mwaka 2014 katika mkutano mkuu wa IPU.
Katika hatua nyingine, Wabunge vijana wametakiwa kuwa
chachu ya maendelo katika nchi zao kwa kushawishi kutengeneza mazingira ya
upatikanaji wa ajira kwa vijana katika kipindi hiki cha uchumi wa kitandawazi.
Hayo yamesemwa jana na Mtaalamu wa maswala ya ajira kutoka
shirika la la kazi la umoja wa mataifa (ILO) alipo toa maada katika mjadala wa
Wabunge Vijana kujadili na namna ya kupunguza ajira kwa vijana hususani katika
kipindi hiki cha uchumi wa utandawazi.
Mtaalamu huyo amesema ni wajibu wa wabunge kuwa na
ushawishi mkubwa kwa serikali zao na baadhi ya taaisisi zinazotoa ajira ili
kuwa na sera madhubuti kwa ajira za vijana hususani wanaomaliza vyuo kwa lengo
la kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.
Amesema hivi saa duniani, zaidi ya asilimia 60 ya watu wote
duniani ni vijana, na wengi wao wanakabiliwa na tatizo la ajira swala ambalo ni
hatari kwa maendelo ya nchi nyingi duniani.
Wakichangia mada hiyo wabunge wengi walikubaliana dunia
kuwa na tatizo la ajira na hususani kwa kushawishi serikali zao kuwa na sera
madhubuti zenye kutatua tatizo la ajira kwa vijana katika nchi zao.
Mmoja wa wabunge kutola Denmark akichangia maada hiyo,
amesema yeye anatoka katika mojawapo ya nchi zenye tozo kubwa la kodi katika
sekata mbalimbali duniani, lakini wao kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa kupunguza
tatizo la ajira kwa vijana kwa kuweka sera mathubudi zenye kuhakikisha kuwa
vijana wanapata ajira mara tu wamalizapo shule.
Anasema moja wapo ya sera hizo ni pamoja na kuwa na kodi
kubwa sana kwa
mashirika au kampuni ambayo hayatoi idadi kubwa ya ajira kwa vijana au ambayo
hayazingatii ajiri kwa vijana. Pamoja na hilo,
serikali ya Denmark
imeweka utaratibu wa kutoa punguzo la kodi kwa mashirika au Makampuni yenye
sera ya kuajiri vijana kutoka vyuoni ambapo hivi sasa ni asilimia 6% tu ya watu
kutoka Denmak hawana ajira.
Tatizo hili limejitokeza sana katika chi za afrika, Asia na
Latini Amerika ambapo Mbunge kutoka Namibia akichangia mada hii amesema
nchini kwake tatizo la ajira ni zaidi ya asilimia 52 na mashirika mengi na
makampuni yanayojishughulisha na biashara kwa lengo la kupata faida, huona ni
hatari sana kuajiri vijana wanaotoka kazini kwa kuwa wengi wao hawana uzoefu
hivyo kufanya swala la uzalishaji kupungua kutokana na mda mwingi kutumika
kufanya mafunzo kazini, jambo ambalo limepingwa vikali na wajumbe kutoka Afrika
kusini, Tanzania, Norway na Maldives.
Mbunge David Kafulila aliyeshiriki semina hiyo kutoka
Tanzania, amesema sio kweli kwamba serikali zetu zitafanya kila kitu kutoa
ajira kwa vijana, akichangia mada hiyo, kafulila alisema “ swala hapa
ni kutengeneza mazingira ya kuwa na soko la ajira kwa vijana mara tu wamalizapo
shule, sasa ni jukumu letu kushawishi serikali zetu kuwa na sera rafiki zenye
kuweka mpango wa kutengeneza ajira kwa vijana” .
Kafulila aliongeza kuwa, mfano ni serikali zetu kuanzisha
mikakati mipya ya maendeleo yenye kulenga kutoa elimu kulingana na soko la
ajira, pamoja na kuvutia wawekezaji katika sekta muhimu zenye kutoa ajira kwa
vijana.
Akitoa mfano wa Tanzania, Kafulila anasema hivi sasa sekta
ya gesi, mafuta na Kilimo Tanzania ndiko soko kubwa la ajira liliko na lengo
lao kama wabunge vijana Tanzania watahakikisha kuwa wanaishawishi sana serikali
kuwa na sera ya jira kwa vijana kwa wawekezaji wote wanowekeza katika sekta
hizi pamoja na kuongeza idadi ya vyuo vyenye kutoa elimu kulingana na mahitaji
ya sekta hizi kuliko kuwa na wataalam wengi kutoka nje wanaokuja kufanya kazi
Tanzania kwa kuwa kuna uchache wa wataalam katika sekta hizi.
Tatizo lililopo sasa ni kwamba nchi zetu ziache utaratibu
wa kuongeza idadi ya vyuo vinavyotoa elimu inayofanana bila kuangalia mahitaji
ya soko, kwani kuwa na idadi kubwa ya wasomi kwa fani moja tu nchini ni tatizo
kubwa katika maendeleo ya nchi.
Mkutano wa 127 wa IPU unaendelea leo hapa mjini Quebec ambapo mojawapo
ya warsha itakayofanyika ni pamoja na ile inayosema “Kinga za Wabunge, ni Mzigo
au ni kwa manufaa?
No comments:
Post a Comment