Maalum kwa habari mbalimbali za kisiasa, kiuchumi, kijamii, michezo na burudani pamoja na matukio.
Wednesday, October 31, 2012
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Hai, Novatus Makunga wakati alipowasili wilayani humo kwa ajili ya uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Hai_Masama mkoani Kilimanjaro. |
Tuesday, October 30, 2012
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
1. Kamati ya Ligi jana (Oktoba 29,2012) ilifanya
kikao pamoja na klabu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom kujadili mambo kadhaa,
likiwemo tukio la Jumamosi iliyopita la kuzuia televisheni na radio kutangaza
moja kwa moja michezo ya Ligi Kuu pamoja na wapiga picha za televisheni
kuchukua picha kwa ajili ya kutumia kwenye habari. Kamati ilifanya mazungumzo
na mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za
Michezo (TASWA), Juma Pinto kuhusu msukosuko huo na kufikia muafaka katika
masuala yafuatayo:
a- kwamba uamuzi wa kuzuia vituo vya redio na
televisheni kutangaza moja kwa moja ulikuwa sahihi lakini una kasoro katika
utekelezaji kwa kuwa hayakuwepo mawasiliano rasmi kwa vyombo vya habari na pia
haukutoa muda wa kutosha kwa vyombo hivyo vya habari kufanya maandalizi kwa
kadri ya utashi wa klabu za Ligi Kuu.
b- Kwamba Kamati ya Ligi haijakataza redio
kutangaza moja kwa moja michezo ya Ligi Kuu, bali vituo vya redio ambavyo
vinataka kutangaza moja kwa moja michezo ya Ligi Kuu vifanye hivyo bila ya
kuweka matangazo ya wadhamini na kama matangazo hayo ya moja kwa moja
yatadhaminiwa, basi vituo hivyo havina budi kuwasiliana kwa maandishi na
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa maelekezo zaidi.
c- Kwamba vituo vya redio vitakavyotaka
kutangaza moja kwa moja michezo ya Ligi Kuu, ni lazima zitamke mashindano hayo
kuwa ni “Ligi Kuu ya Vodacom”.
d- Kwamba vituo vya televisheni vitakavyotaka
kutangaza moja kwa michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom, ni lazima viingie mkataba na
TFF ambao utaaridhiwa na klabu husika. Kwa sasa, kituo cha televisheni cha Star
TV hakitaruhusiwa kurusha matangazo ya moja kwa moja ya michezo hiyo hadi hapo
mkataba utakaposainiwa na tunatumaini mkataba huo utasainiwa kabla ya mechi za kesho
na hivyo kuwapa fursa wapenzi wa soka wa maeneo mbalimbali kuendelea kushuhudia
Ligi Kuu ya Vodacom.
e- Kwamba vituo vya televisheni vitakavyotaka
kuchukua picha kwa ajili ya habari zinaruhusiwa kufanya hivyo. Endapo kituo
hicho kitaonyesha mchezo uliorekodiwa, hatua zitachukuliwa dhidi ya kituo
hicho.
f- Kamati inaomba radhi kwa usumbufu
uliosababishwa na uamuzi huo, lakini inazidi kusisitiza kuwa uamuzi huo
ulifanywa kwa lengo zuri la kuendelea kutafuta vyanzo vya fedha
vitakavyoziwezesha klabu kujimudu kiuchumi na kuifanya Ligi Kuu ya Vodacom
iendeshwe kwa ubora zaidi.
2. Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Kim
Poulsen amerejea Dar es salaam baada ya kufanya ziara kwenye visiwa vya Pemba
na Unguja ambako alishuhudia mechi sita za Ligi Kuu ya Grand Malta kuanzia
Oktoba 19, 2012 hadi Oktoba 26, 2012 visiwani Zanzibar. Poulsen alishuhudia
mechi baina ya Falcom na Bandari iliyoisha kwa Falcom kushinda kwa mabao 3-1 na
pia mechi baina ya Duma na Bandari ambayo iliisha kwa Bandari kuibuka na ushindi
wa mabao 2-0. Mechi hizo mbili zilifanyika kisiwani Pemba.
Poulsen pia alishuhudia mechi
zilizofanyika kwenye Uwanja wa Amaan kisiwani Unguja ambako Mtendeni iliibwaga
Chipukizi kwa mabao 2-1; Mundu na Jamhuri (0-1), KMKM na Zimani Moto (1-0); na
Mafunzo dhidi ya Chuoni iliyoisha kwa Mafunzo kulala kwa mabao 3-0.
Poulsen amefurahishwa na
ziara hiyo na kusema kuwa ni kitu kizuri kwake na kwa soka la Tanzania kwa
ujumla. Poulsen alisema kuwa amefurahishwa na mapokezi aliyopata visiwani Zanzibar na kukishukuru Chama cha Mpira wa Miguu cha
Zanzibar (ZFA) kwa ushirikiano mkubwa alioupata wakati wote akiwa Zanzibar.
Hata hivyo, Poulsen alisema
hawezi kueleza kwa sasa kama ameona wachezaji
anaoweza kuwaita kwenye kikosi cha Taifa Stars, lakini akasema amevutiwa na
viwango vya wachezaji wengi.
3. TFF inapenda tena kuihimiza klabu ya Yanga
kumalizana na mchezaji wake wa zamani, John Njoroge Mwangi kabla ya Novemba 2,
2012 ili ijiepushe na adhabu kaili inayoweza kuchukuliwa na Shirikisho la
Kimataifa la Vyama vya Mpira wa Miguu (FIFA). Kwa mujibu wa barua ya FIFA,
iwapo Yanga haitakuwa imemlipa mchezaji huyo na kusiwepo na mawasiliano yoyote,
shauri hilo
litawasilishwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya FIFA itakayokutana Novemba 14, 2012
kutathmini hukumu iliyotolewa mapema Januari mwaka huu.
4. Mchezo namba 10 wa Ligi Daraja la Kwanza
(FDL) baina ya Morani na Polisi Tabora uliokuwa uchezwe Kiteto mjini Tabora
Oktoba 31, 2012, sasa utachezwa Novemba 01, 2012 baada ya treni ambayo Morani
walikuwa wakisafiria kutoka kupata matatizo njiani wakati wakitoka Kigoma
ambako walicheza na Kanembo.
5. TFF inapenda kutoa ufafanuzi wa taarifa
zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari leo, likiwemo gazeti la Habari Leo
na Daily News, vikimnukuu rais wa TFF, Leodegar Tenga akisema kuwa amewataka
watu wanaotaka kugombea uongozi wa shirikisho watangaze nia ili wapate
kujadiliwa. Waandishi walioandika habari hiyo hawakumnukuu vizuri Rais Tenga
wakati akizungumzia masuala ya uchaguzi na hivyo kupotosha maana nzima ambayo
Ndg. Tenga alitaka iwafikie wapenzi wa michezo na hasa mpira wa miguu. Rais Tenga
alivitaka vyombo vya habari vianzishe mjadala utakaowashirikisha wapenzi wa
mpira wa miguu ili waelezee wanatarajia nini katika miaka ijayo na hivyo
kuwafanya viongozi watakaochaguliwa kufanya kazi kwa utashi wa maoni hayo ya
wananchi. Tunaelewa kuwa Rais Tenga ni muumini wa kuheshimu katiba, sheria na
kanuni na hivyo hawezi kutoa kauli ambayo inakiuka mchakato wa uchaguzi wa TFF
kwa kuwataka wanaowania uongozi kutangaza nia sasa badala ya kusubiri muda wa
kikanuni ufike. Ikumbukwe katika kikao chake na wahariri aliwahi kuulizwa swali
kama hilo na
akasema kuwa akijibu lolote atakuwa amekiuka kanuni za uchaguzi kwa kuwa
itamaanisha anaanza kampeniu kabla ya muda. Ni vizuri waliohusika wakafanya
masahihisho ili kuzuia habari zao kutafsiriwa tofauti na wadau wa mpira wa
miguu na hivyo kuweka uwezekano wa kuvuruga mchakato wa uchaguzi.
6. TFF imebadilisha tarehe ya kuanza kuchukua
fomu kwa watu wanaotaka kugombea uongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Dar es salaam (DRFA) kwa
lengo la kuhakikisha kuwa mchakato wa uchaguzi unafanyika kwa mujibu wa kanuni.
Kamati ya Uchaguzi ya DRFA ilitangaza jana kuwa uchukuaji fomu ungeanza leo,
lakini DRFA iliandikiwa barua jana kuelezwa kuwa mchakato huo sasa utaanza
kesho na uchaguzi utafanyika Desemba 12, 2012.
Mchakato wa uchaguzi wa
viongozi wa DRFA utakuwa kama ifuatavyo:
30/10/2012 Kamati
ya Uchaguzi DRFA kutangaza uchaguzi na nafasi
Zinazogombewa
kwa mujibu wa katiba ya DRFA
31/10/2012 Kuanza
kuchukua fomu za kugombea uongozi
04/11/2012 Mwisho
wa kurudisha fomu ifikapo saa 10:00 alasiri
05-09/11/2012 Kamati ya
Uchaguzi DRFA kupitia fomu za waombaji uongozi na
kutangaza matokeo na
kubandika kwenye mbao majina ya waombaji uongozi.
10-14/11/2012 Kutoa fursa
ya pingamizi dhidi ya waombaji uongozi. Pingamizi
ziwasilishwe
kwa katibu wa Kamati ya Uchaguzi DRFA na
wawekaji
pingamizi wazingatie Ibara ya 11 (2) ya Kanuni za
Uchaguzi za
Wanachama wa TFF.
15-17/11/2012 Kujadili
pingamizi, usaili na kutangaza matokeo ya usaili na
kuwajulisha
kwa maandishi.
18-20/11/2012 Kukataa rufaa
dhidi ya maamuzi ya Kamati ya Uchaguzi ya DRFA
21-25/11/2012 Rufaa
kusikilizwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF na kutangaza
matokeo ya
rufaa (Kama hakuna rufaa, Kamati ya Uchaguzi
ya
DRFA
kutangaza majina ya wagombea na nafasi wanazogombea
na kuanza
kampeni).
26/11/2012 Baada
ya maamuzi ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Kamati ya
Uchaguzi ya
DRFA kutangaza majina ya wagombea na nafasi zao
na kuanza
kwa kampeni
WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI WAGOMA
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Kimnyaki iliyopo wilayani Arumeru wakiwa mbele ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha wakidai kuondolewa kwa Mkuu wa shule yao kwa madai ya kuchelewesha wanafunzi wa kidato cha Nne kufanya mitihani.
Monday, October 29, 2012
TRENI YA ABIRIA YAANZA KAZI JIJINI DAR NAULI NI SHILINGI 400 TU
Abiria treni ya kwanza kusafiri na wakiwa ndani ya treni ya abiria inayotoa huduma zake kutoka Ubungo Mziwa hadi Stesheni jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi. |
USAFIRI WA TRENI KAMA DALADALA WAANZA JIJINI DAR ES SALAAM NAULI NI SHILINGI 400
Abiria wa mwanzo wa kutumia treni kwa usafiri wa ndani ya jiji ;a Dar es Salaamkwa kutumia reli ya Kati wakiteremka katika kituo cha Stesheni nauli kwa kila mtu ni shilingi 400/- |
Treni ya kwanza kuteremsha abiria kwa kutumia usafiri wa kawaida kutoka Ubungo Maziwa hadi Stesheni jijini Dar es Salaam. Usafiri huu utakuwa ni mkombozi kwa wakazi wa Ubungo, Tabata na Buguruni, |
Sunday, October 28, 2012
UMOJA WA VIJANA WA CCM WATWANGANA MANGUMI
Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Vijana wa CCM wakiwa wamemshikilia mmoja wa vijana wanaompinga Mwenyekiti mpya wa Umoja
huo, Khamis Sadifa Juma na viongozi wenzake,
Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Vijana wa CCM wanaomuunga mkono Mwenyekiti wa Taifa wa umoja huo aliyechaguliwa hivi karibu mjini Dodoma wakimpga mangumi mmoja wa wanachama hao wanaopinga matokeo ya uchaguzi huo wa Mwenyekiti huyo kwa madai kuwa rushwa imetembea. Mpambano huo ulikuwa makao makuu ya umoja huo jijini Dar es Salaam
Bondia Rashid Matumla akipima uzito tayari kwa kupambana na Mkenya katika pambano lao lililotarajiwa kufanyika mjini Mtwara.
Friday, October 26, 2012
MELI YA KIVITA KUTOKA UINGEREZA YATIA NANGA BANDARI YA DAR ES SALAAM
Askari wa Uingereza wakinyesha mfano wa namna ya kuwakabili maharamia wakati meli yao inayofanya doria Mashariki ya Kati ilipotia nanga katika bandari ya Dar es Salaam |
ASKARI WA UINGEREZA WA KIKOSI KINACHLINDA USAMA MASHARIKI YA KATI WAWASILI DARESSALAAM NA MELI YA KIVITA
Askari wa Kikosi cha kulinda usalama Mashariki ya Kati wakionyesha jinsi ya kuwakabili maharamia kwenye kwenye bahari. |
A
Askari wa Uingereza kikosi kinachilinda usalama Mashariki ya Kati wakionyesha namna ya kumdhibiti haramia |
Askari wa Jeshi la Maji la Uingereza wanaofanya doria katika ukanda wa Mashariki ya Kati wakionyesha jinsi ya kumdhibiti haramia wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. |
Thursday, October 25, 2012
Mheshimiwa Hamad Rashid ateuliwa kuwa mjumbe kamati ya ukaguzi wa Hesabu za ndani IPU
Wateja wa Airtel sasa kulipia Kodi kwa Airtel Money
KATIBU WA BAKWATA ARUSHA AJERUHIWA
Wednesday, October 24, 2012
AIRTEL YAZINDUA PROMOSHENI YA JIPATIE MARA TANO”
DR SHEIN AKIMPONGEZA MWENYEKITI MPYA WA UVCCM KHAMIS SADIFA JUMA
Dk. Sheni akimpongeza Khamis Sadifa Juma, baada ya kutangazwa Mshindi wa kuwa Mwenyekiti mpya wa UVCCM Taifa, katika uchaguzi uliofanyika mjini Dodoma. |
KHAMIS SADIFA JUMA ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI MPYA WA UVCCMKhamis Sadifa Juma,
Khamis Sadifa Juma, baada ya kutangazwa Mshindi wa kuwa Mwenyekiti mpya wa UVCCM Taifa, katika uchaguzi uliofanyika jana mjini Dodoma. |
Subscribe to:
Posts (Atom)