Monday, May 14, 2012

Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya namtumbo Dkt Simon Chacha na Mkurugenzi wa maendeleo wa wilaya hiyo Mussa Zungiza kulia,wakiwaongoza wageni na watumishi wa idara ya afya kwenda kuwafariji wagonjwa waliolazwa katika wodi mbalimbali katika hositali ya wilaya hiyo, wakati wa sherehe ya siku ya wauguzi Duniani.
Askari polisi wa kituo cha Namtumbo mkoani Ruvuma,wakiongoza zoezi la uwashaji mishumaa kama ishara ya upendo na matumaini kwa wagonjwa na watu wenye shida mbalimbali, wakati wa sherehe za siku ya wauguzi Duniani ambayo kiwilaya ilifanyika katika viwanja vya hospitali mjini Namtumbo,

Sunday, May 13, 2012

Mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya ukandarasi, Paul Kihenge mkazi wa mjini Songea  alikutwa  na pigapicha wetu jana akiendelea na ujenzi wa mfereji wa maji katika sehemu korofi  katika  barabara ya Lundusi wilayani Songea,  mkoani Ruvuma. Kampuni hiyo ya ukandarasi kutoka mjini Songea imepewa kipande katika barabara hiyo kujenga mfreji wa mita 200 pamoja kuweka makalavati  katika sehemu korofi ya barabara ya Lundusi, ambayo ni barabara yanayoelekea katika makao mkuu mapya ya Halmashauri ya Wilaya Songea vijijini yanayoendelea kujengwa katika maeneo ya Maposeni, barabara hiyo inatarajia kutiwa lami baadaye. (PICHA: FRIDAY SIMBAYA)
Mbunge wa Same Mashariki Anne Kkilango akishangaa mashimo ya uchimbaji wa dhahabu  huku akiwa ameshika baadhi ya zana zilizotelekezwa na watu wanaochimba madini ktk msitu wa shengena
picha  na Asraji Mvungi

MH ANNE KILANGO ATEMBELEA MACHIMBO

Mbunge wa Same Mashariki Mama Anne Kilango akishangaa mashimo ya uchimbaji wa dhahabu  huku akiwa ameshika baadhi ya zana zilizotelekezwa na watu wanaochimba madini ktk msitu wa Shengena
picha  na Asraji Mvungi
Baadhi ya wakazi kutoka sehemu mbalimbali mkoani Kilimanjaro na nje ya mkoahuo wakitoa heshima zao za mwisho mbele ya mwili wa marehemu mzee Elitira Abraham Mengi nyumbani kwake Machame Mkuu wakati wa mazishi yake