Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga imeapa 'kufa na kupona' mjini Tanga watakapoumana na Coastal Union katika mfululizo wa ligi hiyo.
Yanga na Coastal zinatarajia kumenyana Jumamosi kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga ambapo kila timu inahitaji ushindi ili kujiweka pazuri katika ligi hiyo inayoelekea ukingoni.